Friday, February 27, 2009

Pandeni Pipa


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


PRECISION AIR YAPUNGUZA NAULI KWA AJILI YA PASAKA


Dar es Salaam, Februari 27, 2009: Precision Air, shirika kubwa la ndege nchini, limetangaza punguzo la nauli kwa wasafiri wanaopanga kusherehekea sikukuu ya Pasaka na ndugu na jamaa zao.

Taarifa hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Meneja Masoko na Mawasiliano wa shirika hilo Annette Nkini. Akielezea nauli hizo mpya, Nkini alisema kuwa kuanzia Februari 15 mwaka huu tiketi ya kutoka Dar es Salaam hadi Kilimanjaro ni Sh. 116,000 na Sh. 179,000 kwa safari nzima ya kwenda na kurudi, wakati kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma sasa ni Sh. 157,000 na Sh. 241,000 kwenda na kurudi.


Kwa safari za nje ya nchi, kutoka Kilimanjaro hadi Entebbe sasa ni $131 na kwenda na kurudi ni $187 wakati wasafiri waendao Mombasa kutoka Dar es Salaam sasa watalipa $151 na $216 kwenda na kurudi.

Nkini aliongeza, “Watu wengi hupendelea kutumia muda wa wikiendi ndefu mbali na miji wanayoishi kwa sababu mbalimbali ikiwemo kujumuika na ndugu na jamaa zao na tunafurahi kuweza kuwasaidia kufanikisha hilo. Punguzo hili la nauli linalenga wasafiri wa ndani na wale wa nje pia. Shirika letu linatoa huduma Afrika Mashariki na hivyo ni muhimu kwa mapunguzo ya nauli kuendana sambamba na uhalisia huo.”


Tiketi zenye punguzo hilo zitaendelea kuwepo hadi Machi 31 na kuweza kutumika mpaka Aprili 30 na zinapatikana kwenye ofisi za mauzo za Precision Air na mawakala mbalimbali.

No comments:

Post a Comment