Sunday, February 22, 2009

Donge Nono PCCB


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) imetangaza kutoa donge nono kwa mtu yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa kigogo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba ambaye anatafutwa kwa amri ya mahakama na haijulikani alipo.


Afisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani amesema wameamua kutangaza doge nono la fedha ambalo hakutaja ni kiasi gani ili wananchi wasaidie kupatikana kwa Liyumba, aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi (DPA).


"Kuna wananchi tumesikia wako tayari kuisaidia Takukuru, tunawakaribisha na Dk Hoseah anawakaribisha ili waweze kutusaidia na donge nono litatolewa kwa atakayefanikisha kukamatwa kwa Liyumba," alisema Kapwani. Soma zaidi

No comments:

Post a Comment