Tuesday, February 24, 2009

Dhamana ya Liyumba yafutwa


'Habari Mpasuko'

Baada ya kutokea mahakamani asubuhi leo, dhama ya Amatus Liyumba imefutwa na sasa amepelekwa Keko kuendelea na dona lake. Documents zake zina utata, pasi yake imeisha muda na baadhi ya mali si za kudumu.
Hakimu abadilika
Hakimu Msongo alisema mahakama iliwasiliana na Idara ya Uhamiaji na kuthibitishiwa kwamba mshitakiwa anamiliki hati nyingine ya kusafiria iliyotolewa Juni 10 mwaka 2005 na kwamba muda wake wa kuisha ni June 2015 wakati mtuhumiwa huyo aliwasilisha mahakamani hapo hati ya kusafiria iliyoisha muda wake ambayo inaonyesha inamaliza muda wake Desemba 12 mwaka 2007.

No comments:

Post a Comment