Thursday, January 22, 2009

"Untold' Pictures!

Nenda Mwalimu: Obama na mkewe pamoja na Biden na mkewe wakiipungia helkopta iliyombeba Bush kuondoka White House kwenda baada ya kumaliza kazi ya kuiongoza nchi hiyo. Safari hiyo iliishia katika uwanja wa ndege wa Jeshi alipoparamia pipa Air Force (one) kuelekea Texas
Hapo patamu sana: Ndivyo anavyoelekea kuwaza George Bush na mkewe, walipokuwa wanapungiana mikono na familia ya Rais mpya, Obama.

Mungu Nisaidie; Obama akisubiri kuitwa nje walipo watu karibu milioni mbili kwenda kuapishwa.


Itakuwa Hivi: Obama na mkewe wakifanya zoezi jinsi watakavyoapishwa. Hii ilikuwa muda mfupi kabla ya tukio hilo Jumatano iliyopitaImekaa Sawa: Obama akijiangalia kwenye kioo kuhakikisha kama anaonekana sawa sawa, muda mfupi kabla hajaingia kuapishwa. Ingewa habari, tungesema hii ni Untold Story, sasa ni pisha, sijui tusemeje.
No comments:

Post a Comment