Tuesday, June 10, 2008

Zombe Leo

Abdallah Zombe akiongea na wakili wake, Maira
Umati wa watu wakiingia mahakamani kusikiliza kesi maarufu kwa sasa ya Zombe na wenzake 12. Ifuatayo ni sehemu ya Ushahidi wa leo:Na James Magai
SHAHIDI wa 27 katika kesi ya mauaji ya kukusudia ya wafanyabiashara watatu wa Madini wa Mahenge Morogoro, na dereva teksi jana aliieleza Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam kuwa mshitakiwa wa pili katika kesi hiyo, Mrakibu wa Polisi (SP) Christopher Bageni aliamuru askari polisi kuwafyatulia risasi wafanyabiashara wa madini wa Mahenge
.

Akitoa ushahidi jana katika mahakama hiyo, Kamishna Msaidizi wa Polisi Kitengo cha Upelelezi Makao Makuu ya Polisi (ACP) Maximinus Michael alidai SP Bageni alitoa maagizo hayo baada ya wale wafanyabiashara waliouawa kwa tuhuma za ujambazi kuwarushia risasi polisi. (haya ni maelezo kuhusu eneo la Sinza, si Msituni Panda)

No comments:

Post a Comment