Friday, February 08, 2008

Taarifa za Uhakika

JK amekubali ombi la kujiuzulu la Dk Edward Hosea (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru kuanzia saa 6.00 mchana leo. Anayekaimu ofisi hiyo nyeti, ni aliyekuwa naibu wake, Lilian Mashaka. Takukuru imetajwa kwa kuwalinda watuhumiwa wa ufisadi katika kashfa ya Richmond. Katika Kashfa hiyo kiongozi aliyetajwa na hajajiuzulu hadi sasa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, ambaye bila shaka alibakia ili kukamilisha kazi ya Rais ya uteuzi wa Waziri Mkuu na taratibu za kutangazwa kwake; na pengine kuapishwa kwake.

No comments:

Post a Comment