Monday, June 05, 2006

Sikio la Serikali Hili Hapa: Weka Maoni Yako

Nimeivumbua. Ahadi ya serikali ya Awamu ya Nne kuwa itaanzishwa tovuti ya serikali ambapo wananchi walio ndani na nje ya nchi watakuwa wanaweka maoni yao (sina hakika kama na wasio wananchi wanaruhusiwa). Serikali yao, kupitia Rais JK ilisema itakuwa inayachukua na kuyafanyia kazi. HII HAPA kazi kwenu.

6 comments:

Reggy's said...

Kadri ninavyoamini hii site ni serikali. Ilitangazwa na Rais Jakaya Kikwete miezi kadhaa iliyopita, kuwa itaanzishwa ili kukusanya maoni ya wananchi juu ya masuala mbalimbali. Inavyoonekana imekusanya taarifa za ndani na sahihi za serikali, labda kama wajanja wametumia mlango huo, hapo ni vigumu kuthibitisha.

ARUPA said...

Bado sina imani kama itatumika kadri ya malengo yaliyowekwa kwani nahisi wasiotakiwa wataitumia visivyo wavuti hii.lla nashukuru kwa kutukumbusha sie wasomaji ahadi hiyo iliyotolewa na mkuu wetu wa nchi wakati anaomba kura zetu.

Jeff Msangi said...

Shukrani kwa kutuletea wavu huu.

Jeff Msangi said...

Shukrani kwa kutuletea wavu huu.

Rama Msangi said...

Nadhani huu sio WAVU kwakweli bali KOKORO (Miruko nadhani unayajua mmeshakamata mengi kule Mtera) maana nahisi kama litakusanya mpaka vile visivyotakiwa. Sina hakika kama KOKORO hili halijaanzishwa kwa malengo maalum kama yale maswali aliyokuwa akiulizwa JK wakati wa mchakato wa kumpeleka katika pepo aliyopo sasa, maana naambiwa yalikuwa maswali yenye mlengo maalum

Reggy's said...

Mimi nadhani wavu ni sahihi zaidi kumaanisha anachomaanisha Msangi mkubwa (Jeff). lakini hili kokoro la Msangi Mdogo linanipa wasiwasi, kwani tukiliruhusu litasomba kila kitu; samaki babu, baba, mama, kama , dada na 'mayai'. Matokeo yake hii itakauwa kinyume na maazimio yetu, likiwemo la Dodoma, kwani tunatakiwa kufanya kile watalaamu wanaita 'self censorship'

Post a Comment