Tuesday, April 25, 2006

Mavuno ya Bangi: Kama si hivi wafanye kazi gani?

Bangi0
Hivi karibuni Polisi wa Dodoma walifanya 'operesheni' ya kusaka mashamba ya bangi, kuivuna na kuiteketeza kwa moto. Bangi imepandwa katika safu za milima mirefu 'kama vile torabora Afghanstan. Sina hakika kama watafanikia. Picha hii 'imechezewa' kidogo ili kuleta matukio tofauti ndani ya picha moja. (Picha na RSM)

3 comments:

Habari Hub said...

Reginald

Hawawezi kufanikiwa hao polisi si unajua hii kule kwao Nyaronyo Kicheere ni mboga ya majani na ni halali kwao, wanadhani ina faida kibao sambamba kiburudisho pia.

Sasa hapa kuna conflict of interest bangi kama mboga na vile vile kama madawa ya kulevya itafutwa vipi!

boniphace said...

Charahani suala la bangi latakiwa kutazamwa na kujadiliwa maana limesaidia wengi kusoma lakini kuna madhara ya sigara na hilo bangi kwa afya za sisi tusiovuta na hasa ukija kwenye Kansa. Bora tuifutie mbali hii mibangi na misigala maana sisi tuliozika watu wetu kwa Kansa tunajua uchungu huu.

Anonymous said...

Nice! Where you get this guestbook? I want the same script.. Awesome content. thankyou.
»

Post a Comment