Nimepokea waraka Pepe huu kutoka kwa asiyependa kujitambulisha. Unamhuru Dk. Mathayo David, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko. Unaweza kusoma HAPA kuna mdahalo wa utata wa PhD yake na wenzake. Pia umetumwa kwa waandishi wengi wa habari, na gazeti moja la Tanzania Daima limeshatumia story yake. Tafadhali Usome hapa chini.
By Anonymous Writer
A Tanzania deputy minister may still be drawing a salary from Botswana government almost eight months after he returned to his native country. Authorities were this week sent in to a frenzy at the shock revelation that Dr. David Mathayo David (37) who was employed as a lecturer in agriculture at the Serowe College of Education, was in fact paid to fund his political campaigns last year.
College Principal Caiphus Dema said they did not know that David was involved in politics. "What we know is that he went on a three week sick leave last year in June. He said he wanted to be close to his family. When the leave was over he applied for an extension a number of times saying he was still very sick," Dema said.
A reliable source has alleged that David is still on government payroll. "He is still getting paid as he is still considered an employee of the college," she said.
Nevertheless, Dema said he doubted that David was still getting paid. "He said he was considering resigning as he was too sick to work," Dema said. He said when he did not return, they went to his house sometime last year to reclaim the school furniture. "It did not appear as if he had left any of his belongings," Dema said.
David became a Member of Parliament for Same Magharibi (West) constituency under the ruling party, Chama Cha Mapinduzi ticket after the October parliamentary elections. He was subsequently appointed Deputy Minister of Industry, Trade and Marketing December 28 last year.
Approached for comment, the Teacher Service Management (TSM) referred us to the Department of Teacher Training and Development.
The Deputy Director, Tebogo Mongatane, requested a questionnaire last week saying she feared being misquoted.
She had promised to answer the questionnaire as soon as it was sent. Nevertheless, a follow-up on Friday afternoon found she had 'other important obligations.'
On Monday afternoon she sent a response advising us to "direct these questions to TSM, who are employer and are responsible for all employment matters affecting teachers."
Efforts to reach David for comment proved futile.
Writers Commnets…
Hii habari inatia woga kidogo. Ukiisoma inaonyesha Naibu Waziri sio mkweli. Alimdanganya mwajiri wake kuwa anaumwa kumbe yuko kwenye harakati zake za kisiasa. Hapa kidogo panatia shaka kama hatamdanganya Mheshimiwa Rais kwenye wadhifa wake mpya alionao mradi mamboyamwendee. Huyu jamaa kuna sehemu nyingine wanamjadili pia, wanasema elimu yake iliyoonyeshwa kwenye website ya bunge sio kweli. Naanza kuamini kuwa hata kwenye sifa zake ametia chumvi kama style yake ndio hii. Nanukuu "Mh. Mathayo David Mathayo (naibu waziri wa biashara na viwanda), alisoma SUA degree ya wanyama (Bachelor Vet. Medicine) kati ya 1992-1997 na tulikuwa tunakaa naye Hall moja pale na nilimwacha pale, na baaada ya hapo alifanya kazi kidogo Botswana na akarudi nyumbani kujiunga na NECya CCM (kutokea kundi la vijana), sasa cha kushangaza hivi sasa ana PhD ambayo haijulikani kaipatia wapi na lini, mwanzo nilifikiri wanamwita Dr . kutokana na field yake wanyama kumbe nilipopitia CVs za wabunge, nimegundua naye kapata PhD from Free State University(kwa kifupi hii universityhaipo ni feki-jaribuni ku-google wenyewe). Tena kwa kifupi hana hata Masters degree jamani, sishangai kupewa wizara nyeti bali kinachoikumba Kenya kipo njiani kuja Tanzania, hii ndiyo labda kasi ya kundi la vijana katika kujiingiza kwenye siasa kwa mbwembwe za kwamba waonekane wasomi haswa"
8 comments:
aaahhhhh hapa umeme lazima umekufanyia kitu mbaya! lakini nadhnai ulitaka kuendelea kumnyima raha Kapuya! niliishamnyima raha pia hapo nyuma kidogo!
mark
Hapana si umeme, leo walau ninao, lakini article yenye ilikuwa inagoma kidogo, sijaelewa sababu
Miruko safi sana kutupa hii huyu anapaswa kufanyiwa forum ya nguvu ili aondoke katika kikosi cha JK wakati wa uchunguzi wa taarifa hizi za elimu yake. Kama kweli anakula mishahara miwili kwa uongo hapaswi kuongoza tena huyo, tena kuna suala la elimu hilo ni muhimu na ukitazama wabunge wengi wameweka maelezo ya chumvi katika CV zao nitapitia nami kutazama mmoja baada ya mwingine.
Miruko heko. 'Hii maneno' ndio mimi nataka. Hakika sasa umeleta sebuleni kitu ile roho inapenda. Sio roho kikorosho, hapana. Roho ya maendeleo chanya na pevu. Tutaendelea vipi ilhali tuna viongozi waongo na wezi (kwa kudanganya elimu na kudhulumu serikali za Afrika mbili kwa kuchukua mishahara kote).
Hebu nyie mlio na nafasi magazetini huko fanyeni kuanika uozo huu hadharani na kuupigia upatu. "Agende" -Kiganda kumaanisha 'aondoke'.
Hii ndio maana ya vijana kushika hatamu? Yafaa nini kuwa na vijana waongo na wezi badala ya kuwa na wazee wazoefu na wakweli, walau kwa taaluma zao.
kwa kweli huu mjadala ni wamuhimu sana. Nchimmbi ninamkumbuka akiwa anamaliza Mzumbe wakati huo walikuwa hawajaanza kutoa degree, hivyo kama alimaliza ilikuwa ni advance diploma. kutokana na profile yake kuwa juu kisiasa, moja kwa moja aliingia kwenye siasa kuongoza umoja wa vijana ambapo tulikuta teyari ni PhD holder! kwa kweli UZAUZA hili bado sijapata jawabu! - ni kipindi kidogo sana kupata Msc na PhD tena wakati huo huo unafanya siasa! mimi tangu nimalize chuo kikuu shahada ya kwanza 2000 hadi leo bado nahangaika na shule na sioni hiyo PhD itatokea mlango gani!
siyo huyo pekee nakumbuka pia wakati tuko chuo kikuu pale SUA kuna bwana mmoja alimaliza degree ya mifugo kwa jina Azizi Msuya. alibahatika kuingia kwenye halmashauri kuu kupitia umoja wa vijana! huyu lakini wanasema alipojitambulisha alianza na Dr. so and so na wazee wakachanganyikiwa wakisema duh huyu bwana mdogo kamaliza PhD ndiye anatufaa! akaupata na akarudi botswana - alikuwa anafanya kazi botswana! hivyo pia kuna mazingira ya kujilengesha. nasikia pia hata kina marehemu Kighoma Malima ni nyerere akikuwa anawabatiza hizo degree (alianza kumuita profesa vipi profesa nao wakalichukua kama lilivyo)!
Waziri wa Sayansi na elimu ya juu ni mtu mkali sana! namfahamu Profesa Peter Msolla kwani amekuwa ni Naibu Makamu Mkuu wa SUA kwa kipindi na tulifahamiana nikiwa mwanafunzi wake na kiongozi katika serekali ya wanafunzi. tulifahamiana vizuri kwani kuna wakati nikiwa waziri wa usafiri na yeye akiwa mkuu wa taaluma ilibidi tufanye kazi kwa karibu sana. hana mchezo na VIWANGO vya TAALUMA. juzi alisema kuwa wenye degree fake kukiona, lakini sina uhakika kama akiingia anga hizi hatachapwa na vimemo!
lakini ndugu wapendwa. degree ya kutafuta ulaji mwisho ni ya pili (MSc). unapojipa PhD ni kwamba watu wanakusikiliza ndani na nje ya nchi na wanakupa dhamana ya kuwaamulia mambo yao! tuchukulie mfano Prof. Haidari Amani ambaye watanzania tuna imani naye kwani yupo ndani ya tume ya kuweka sawa mchakato wa jumuiya ya Africa Mashariki! sasa watu wakikuomba uwashauri na wewe ukawapa sumu si unatuua wenzio? na kuna haja gani kupata degree na haswa ya udaktari ambayo huwezi ukafafanua mambo? je kwa namna hiyo tutafika? labda ndio maana kukimbilia kwa politiki kwani huko hakuna kuact in a proffesional way? tanzania tukitaka kufika inabidi upuuzi huu na ufe, hakuna jinsi! una PhD sasa so what? mbona nigeria kila mtu karibu anayo? mbona tumemwona JK anafanya kazi yake bomba na digrii yake moja na akawapeperusha PhD na Prof. kwenye kinyang'anyiro? tulimuona Mrema akifanya kazi ya kutukuka na Diploma yake! Mh. Prof. Peter Msolla fanya mambo, anzia huko huko juu!
mark
kupitia gazeti la The Citizen, Dk. Mathayo amekanusha kulipwa mara mbili; Tanzania na Botswana, inasemekana mkataba wake Botswan uliisha Septemba mwaka jana.
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza kwa taarifa yako Marehemu Profesa Malima ana PHD ya Economics kutoka Princeton University na alitunukiwa mwaka April 1971 kama unautata waandikie pale Princeton University watakwambia kuhusu hilo
Kuna watu wengi ni wajinga. Huwa wanaingilia hoja wasizozijua.
Ni upuuzi mtu kusema kwamba eti hakuna Free State university.
Hebu ingia katika;
University of the Free State / Universiteit van die Vrystaat ...UOFS official website detailing the facilities and courses offered by this Bloemfontein based South African university.
www.uovs.ac.za/ - 21k - Cached - Similar pages
Faculties - www.uovs.ac.za/fakul.php
Prospective students - studentportal.uovs.ac.za/
Academic Programmes - www.uovs.ac.za/apps/yearbooks/index.php
Staff Directory - www.uovs.ac.za/apps/staffdirectory.php
More results from www.uovs.ac.za »
Post a Comment