Thursday, February 23, 2006

Wanablog Wakutana na Waziri Mkuu

Hapa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward
Lowassa (kushoto) akisalimiana na mwanablogu, Reginald S. Miruko wakati wa hafla aliyoiandaa kwa ajili ya waandishi wa habari waliokuwa wanaandika habari za Bunge. Hafla hii ilifanyika katika makazi ya PM mjini Dodoma February 17, 2006. Anayeshuhudia katikati ni mwanablogu mwingine Ansbert Ngurumo. (Picha na Deusdedit Moshi)

6 comments:

mark msaki said...

huyo jamaa ni mwanaume anajua maana hasubiri kuambiwa maana. cha maana awasaidie waandishi kutetewa maslahi kwa waajiri wao ili wasinunulike kirahisi na hivyo kufanya kazi inavyotakiwa!

Boniphace Makene said...

Miruko vipi ulimkumbusha kusoma Blogu na ikiewezekana na yeye kufungua yake ili tuweze kutoa maoni kwake? Na pili ni huyu Ngurumo naona uliweza kumrejesha kwa kuwa mlikuwa wote Dom sasa amerudi Dar ndio tusahau au umepanga mkakati mbadala wa kuhakikisha hapotei na kuwa anapatikana wakati wa warsha na semina tu?

mark msaki said...

du kwa kweli huyu mwanaume anapiga mzigo. hii ni picha yake ya pili baada ya kuapishwa namuona akiwa amekonda! pole sana Ngoyai nchi ilikuwa imeishafika kubaya! vijana wako tuko gado ukitaka tafu! ukumbuke na kupumzika pia!

John Mwaipopo said...

Ntamfikishia salamu zako Mark maana naona unamkubali 'kwel-kwel'

Reginald S. Miruko said...

Makene, Huyu bwana nilimweleza uso kwa uso maana tulikuwa owte Dodoma. Pili, nina kawaida ya kuwasiliana naye kwa simu, hasa kila J'2 baada ya gazeti analohariri la Tanzania Daima Jumapili kutoka.

mark msaki said...

Nitashukuru Mwaipopo! kwa kweli ninamkubali!

Post a Comment