Wednesday, February 22, 2006

Eti JK Anawajua Walarushwa! Anangoja Nini?


* Mahita Awasilisha Hati Kustaafu...

Magazeti ya Tanzania leo yamesema mambo makubwa mawili makubwa. Moja kuwa Rais JK Anawajua Walarushwa, anasubiri wajirekebishe. wakishindwa ndo atalazimika kuwataja na kuwashughulikia. Mimi najiuliza, wakijirekebisha watakuwa safi kwa rushwa ambazo wameshakula? Tafakari!

Pili, kwamba Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) , Omari Iddi Mahita, Ameshawasilisha Hati ya Kuomba Kustaafu, kama unavyoandika Mtandao wa www.darhotwire.com unavyoripoti. Gazeti la Daily News la hapa leo Feb 22, 2006, limesema Rais JK ameikubali hati hiyo na kumruhusu Mahita kustaafu ifikapo Machi 4, 2006. Je asubiriwe hadi tarehe hiyo au bado iko mbali? Jiulize!-RSM-

4 comments:

John Mwaipopo said...

Kutunziana heshima na/ama kusamehe yaliyopita ndiko kulikochukua nafasi katika yoote mawili.Kwa hao wala rushwa nina kigugumizi kidogo lakini huyu jamma wa Chuo Cha Upolisi Toronto siku zake zinahesabika. Yawezekana umbumbumbu ndio uliomfanya achemshe.Tumsamehe tu. Si badaye sana atakuwa nje na tutamsahau buriani.

Indya Nkya said...

Huyu hawezi kusameheka Mwaipopo. Tutamsameha kwa kuropoka lakini kwa kuongoza ujambazi wa nguvu na wa kalamu hawezi kusamehewa lazima afilisiwe. Kam JK kweli anasubiri watu wajirekebishe atangoja sana!!

mark msaki said...

na kingine zaidi kumwaga damu zisizokuwa na makosa za wananchi wenzetu! pia kuvuruga demokrasia changa na hivyo maendeleo yetu! unadhani damu aliyomwaga itaacha kutusumbua kama taifa daima?

Ansbert Ngurumo said...

Haya ndiyo ya wabongo - kulindana. Mla rushwa lazima awajue wala rushwa. Lakini hawezi kuwashughulikia. Sana sana ni kuwashtua kidogo ili wasichafue sana awamu yake.

Si mlimsikia Kikwete mwenyewe Jumamosi Machi 4, 2006 akisema kwamba sasa anapendekeza Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitafute njia ya kupata MAPATO HALALI?

Anajua na anakiri kuwa mapato ya chama yaliyomfikisha pale alipo si yote halali. Anajua pia kuwa pale chama kinapopata asilimia 30 za 'mfadhili' mchafu, mtu huyo huyo hubaki na 70. Na wakati mwingine hizo no sehemu tu ya mapato yasiyo halali au rushwa.

Nadhani rais amekuwa muungwana. Hataki kuuma kidole kinachomlisha. Kwa tafakuri yangu, hii ndiyo maana ya yeye kuwapa watu hawa muda wajirekebishe! Mnasemaje?

Post a Comment