Saturday, February 25, 2006

Blogu za Picha Zaongezeka

Kweli Athuman moto wa kuotea mbali, nimemtembelea baada ya kuelekezwa na Makene. Picha anazo nyingi na nimemshauri atuwekee nyingi zaidi, na hasa zisizohusiana tu na siasa, kama inavyoonekana kwenye album yake. Kwani picha zake nyingi, nzuri, ni za kampeni za CCM. Mfano, picha hii niliyoipata kwa Athumani, ni waandishi wa habari, ambao kwa vyovyote walichangia kwa kiasi kikubwa JK kushinda Urais kwa kishindo

6 comments:

Boniphace Makene said...

Miruko nilitaka kuandika jambo fulani kwa Athumani nikastahi kwa sababu unapomkaribisha mtu mstahi. Sianze kwa maswali mazito, lakini naweza kuuliza picha hii kupitia kwako, hawa ni waandishi wa CCM au waandishi wa Habari Tanzania. Mbona wametinga viwalo vya CCM kabisa au ndiyo inayofafanua uwazi wa vyombo vua habari Tanzania? Je waliokuwa wanaandika habari za CUF na CHADEMA na TLP na kwingineko nao walikuwa wakitinga viwalo vya vyama hivyo. Kuna swali kubwa hapa kwa mtu mwenye macho mapana kuhusu uhuru na utambuzi wa umuhimu wa Habari bila kujipinda na upande wa kuhabarishia.

John Mwaipopo said...

Siasa za Bongo hizo. Hao wakina Kasumuni wala hawakuambiwa na mtu wavae hivyo. Kujipendekeza tu ili huenda Papa Mukulu akishinda asiwasahau atakapokuwa akihitaji mwandishi wa longolongo zake.

Reginald S. Miruko said...

Bwana Makene, bora umetambua nia yangu ya kuweka picha hii. Hata hivyo, sikubahatika kupata inayoelezea wasiwasi wako kwa ufasaha. Umeshangaa ya musa, sijui ingekuwaje kwa ile ya filauni, kama ungeona jinsi 'waandishi' wote walivyokuwa wakivaa njano na kijani (bila kuchanganya kama hawa).

Mosi, mbali na mavazi, waliamua kuandika makala na habari tu za kumpamba mgombea wao, na pia walimuunga mkono hata kwa mazungumzo ya mitaani.
Pili, wote walikuwa wanalipwa na chama cha mgombea wao posho ya kila siku ni sh 50,000 kwa muda wote wa kampeni, na mahali pengine walikuta matajiri wameshalipia nyumba za kulala wageni na chakula.
Tatu, waliodiriki kuandika kinyume na matarajio ya chama au mgombea, waliondolewa na kurejeshwa katika newsroom
Nne, inasemekana kuna baadhi ya waandishi wanaotarajia kupewa madaraka makubwa katika nafasi mbalimbali za uteuzi wa rais. Tusubiri tuone.

Boniphace Makene said...

Miruko nadhani bado nia ya kutafuta hiyo picha ipo. Tunahitaji kuwa na kumbukumbu hiyo yaweza hata kutusaidia kama kielelezo katika vitabu tutakavyotunga au kuwajua watu wasivyothamini kazi zao na siku watakapopewa zawadi tuwe na pa kuanzia kuhukumu baada ya kuboronga. Natoa hoja mheshimiwa Miruko endelea kututafutia hiyo picha kisha uianike hapa.

Reginald S. Miruko said...

Bwana makene, nadhani hapa utanikubali. Ingawa tukio lenyewe limeshapita na hatuwezi kulirudisha nyuma kupata picha tunazokusudia, lakini hii walau inaonyesha suala lenyewe tunalojadili. Cheki hapa: www.rsmiruko.blogspot.com/2006/02/waandishi-wa-habari-na-mgombea-wa-ccm.html

Anonymous said...

Miruko, umesahau mambo ya Agenda setting na Partisan Journalism wakati wa Chaguzi? Nishasema TZ hakuna Media na hili linatokana na kwamba hata baada ya Uchaguzi bado Media zote(hata zile tulizokuwa tunaziamini)zinafanya kazi ya ku-glorify the status quo! hali hii itafanyua kwa kipindi cha miaka 10 media zisiwe na mwelekeo mwingine, tungojee baada ya kipindi hiki kuwapiga msasa waandishi ili mrudi katika taaluma yenu baada ya kuiua kwa kipindi hiki,INASIKITISHA SANA.

Post a Comment