Monday, February 27, 2006

Waandishi wa Habari na Mgombea wa CCM

Picha hii nimeipata kwenye Album ya Athuman, ikiwa na maelezo yafuatayo: Rais Kikwete, akisalimiana na waandishi wa habari alioambatana nao katika kampeni Kanda ya Kaskazini. Hapa ni katika Uwanja wa Ndenge wa kimataifa wa Kilimanjaro.

4 comments:

boniphace said...

Nashukuru sana sana Miruko. Hivi mnangoja nini ninyi wanablogu kuongza dola? Kwa kasi hii ya kutumana mambo na kuyapata kwa wepesi kiasi hiki mnanipa picha kuwa mwaweza kabisa kuigeuza Tanzania kama Ulaya. Miruko na Jeff na Mark ninyi ni askari wa kwelikweli maana kwa siku hizi za karibuni mmeweza kuendesha agenda kwa spidi mno. Naanza kuona umuhimu wa wazo la Michuzi kuhusu kuunda nchi ya wanablogu ili watendaji wetu wema hawa tuwape hata tuzo siku moja. Ndesanjo upooo

boniphace said...

Miruko huyo ni mwandishi wa chombo kipi? Nimewaona ninaowafahamu na wote wana kofia za CCM. Naomba nifahamishe kwanza huyo aliyetinga fulu viwalo vya CCM maana kuna makala ninaiandaa hapa.

Anonymous said...

nilitaka kucheka hapa Makene! maana mgombea wa CCM katinga tofauti na kinyume na ilivyotakiwa kwa na mwandishi wa habari....

lakioni kitu kimoja ninachokiona kuwa ni credit kwa JK ni kuwa haendekezi magwanda ya kijani... yeye hutoka kiserekali haswa!
! nadhani amegundua kuwa ukianza kuyaendekeza yale magwanda na wazembe watadandia humo humo!!

Makene! hii ndiyo nguvu ya gazeti tando! muda si muda watu wataancha kusoma magazeti bandia na kusoma haya Magazeti Tando!

mark

Reggy's said...

Makene, usiwashukie tu waandishi wa habari wenye sare. Angalia pia, mpiga picha aliyeandika caption hii, akimtaka Kikwete kama Rais wakati alikuwa kwenye kampeni na Rais alikuwa Benjamin Mkapa. Pia, vyombo vyao vilivyokuwa vinachapisha habari zao

Post a Comment