Saturday, February 25, 2006

NOTES: Naweza Kupotea kwa Muda

Sitaki kufanya kama Michuzi. Sitikisi kiberiti wala siwa-bip wasomaji wangu. Ni HALI HALISI. Mgao wa umeme Tanzania umeongezwa makali, ulikuwa saa 12 kuanzia saa 1.00 asubuhi hadi saa 1.00 jioni. Sasa serikali imetangaza kuongeza saa 2 zaidi, yaani hadi saa 3.00 usiku. Sababu ni upungufu wa maji ya kuzalisha umeme wa maji (hydro). Kwa mji mdogo kama Dodoma, huduma za mawasiliano ya kompyuta kama hii, si rahisi kupatikana baada ya saa 3.00 usiku. Hivyo nanyanyua mikono, ninaweza kushindwa kukuletea uhondo kutoka hapa "Makao Makuu", labda kwa kubahatisha. Hadi lini? hadi umeme wa uhakika utakaporejea-RSM-

4 comments:

Anonymous said...

pole sana miruko! baadaye kidogo na mie nafikiria kuingiza timu bongo! kwali ni kasheshe! nafikiria kununua solar system kwa ajili ya kiota changu kabisa!kwa ukweli wa kujua homu hakuna mtandao historia haitaepukika!

mark

John Mwaipopo said...

Pole Miruko lakini twajua uko nasi kimwili na kiroho. Hivi huko Bongo huu si ni wakati wa mimvua kibao? Sayansi ya maji na umeme inakwendaje? Itakuwa vipi itakapofika mwezi wa nane na wa tisa wakati hakuna mvua kabisa?

Reginald S. Miruko said...

Mambo ya mwaka huu ni tofauti. Mvua za vuli hazikunyesha katika mikoa karibu yote 26. Kila kona kuna ukame, na kwa maani hiyo njaa.Mvua za masika zinazotarajiwa kati ya machi na Aprili labda, kama zitanyesha, ndizo zinatarajiwa kuwa mkombozi. Vinginevyo ni njaa na mgao wa umeme kwenda mbele...Tayari serikai imeshaomba jumuiya ya Kimataifa kusaidia tani 100,000 za mahindi (bila mboga) kwa ajili ya kulisha wenye shida zaidi ya milioni 3.

John Mwaipopo said...

Nimefurahia hiyo 'bila mboga'

Post a Comment