Tuesday, February 07, 2006

Viongozi Wote TZ Kuzikwa Dodoma

Bunge la Kwanza la Jamhuri ya Tanzania (Mkutano wa Kwanza baada ya ule Maalum wa Kuapishana na kumchagua Spika) linaanza leo Feb 7, katika ukumbi wa zamani wa Bunge mjini hapa Dodoma. Ukumbi mpya umeshindikana kumalizika kwa sababu ambazo hazijaelezwa. Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo wa siku 14 utajadili Muswada wa Sheria ya Maziko ya Viongozi wa Kitaifa. Muswada huo ukipita, viongozi wote wa Kitaifa, Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge na jaji Mkuu (na wastaafu ambao hawajafa) wakifa watazikwa Dodoma na makaburi yao yatalindwa na Jeshi na Wananchi wa Tanzania (Article 18 (1) (2) na (3). Kwa hiyo 'Saint' Nyerere atabaki peke yake kule Butiama, Mara; Edward Moringe Sokoine, atakuwa kwake Monduli Juu, Arusha na Dk. Omari Ali Juma atakuwa kwake Pemba.Period.

No comments:

Post a Comment