Wednesday, February 08, 2006

Michuzi si Kaidi, AMERUDI

Issa Muhidin Michuzi, mpiga picha mzoefu na mahiri, Februari 6, 2006 alisababisha kizaazaa kwenye blogu pale alipowaaga wanablogu (Soma hapa) kuwa ameachana na blogu na kwenda mtandao mwingine wa www. mbongo.com. Wengi walichangia maoni wakitaka asiondoke kwa sababu picha zake wanazipenda. Sasa amesikiliza kilio cha wengi na kuamua kurejea uringoni kwa wanablogu na kuwaomba radhi, pata taarifa yake.

No comments:

Post a Comment