Tuesday, February 14, 2006

Nani Kama Omar Mahita?

Hakuna mtu anayejadiliwa Tanzania kama huyu, Inspekta wa Polisi (IGP), Omar Mahita Idd. Mjadala umepamba moto dhidi yake, kila mtu akitaka ajiuzulu kwa kushindwa kukomesha ujambazi na uhalifu wa kila aina.
Yeye amesema hatajiuzulu ng'o hadi atakapostaafu Machi mwaka huu. Zaidi, amesema ujambazi nchini unapangwa na Chama cha Siasa cha Civic United Front (CUF) ili kumhujumu kwa kuwa alikikosesha ushindi katika uchaguzi uliopota. CUF wamepanga kuandamana Jumamosi kumpinga na kushinikiza ama ajiuzulu au afukuzwe na Rais.
Rais Jakaya Kikwete mwenye mamlaka naye hajasema lolote, zaidi ya kutaja tu kuwa wapo polisi wanaoshirikiana na majambazi. Labda Rais hataki kumchukulia hatua ili asionekane kaelekezwa na magazeti. Wewe unaonaje?

9 comments:

Mija Shija Sayi said...

Nimekutana na habari Darhotwire kwamba Rais itabidi afanye maamuzi magumu kwa vigogo kwa manufaa ya wananchi.

Habari yenyewe hii chini-:

Maamuzi magumu yaja -JK
Rais JK ametonya japo kidogo tu kuwa, itabidi atoke upya tena kwa namna itakayokuwa na machungu kwa baadhi ya vigogo kwa manufaa ya kitaifa.

JK alimwaga siri hiyo mbele ya wazee alipokutana nao mjini Dodoma hivi karibuni.

Alitonya kuwa ukiwa kiongozi lazima ukubali kufanya maamuzi. Mengine ni magumu mno na ambayo hayatapokelewa vizuri na wachache lakini lazima yafanyike kwani ni kwa manufaa ya Wabongo wote.

Hata hivyo hakufafanua kuwa ni maamuzi gani atakayochukua yatakayomwezesha kwenda sambamba na msemo wake wa Ari mpya.......

Lakini kutokana na list ya vimbembe anavyokabiliwa navyo JK ni pamoja na hiki cha kumwengua/kuengua IGP Mahita ooh sorry ujambazi unaotesa vibaya sana kila kona hapa nchini.

Vingine ni suala la rushwa katika sekta mbalimbali serikalini, ukame na njaa na ukurutu wa ukiritimba ulioota mizizi serikalini.

Hadi sasa Wabongo kibao wamefurahiswa na jinsi JK alivyoainisha utekelezaji wa sera za CCM kama Rais wa awamu ya nne.

Boniphace Makene said...

Miruko hiyom picha inatunyima usingizi maana anaonekana jambazi huyu kabisa akiandaa mpango wa kuvamia benki nyingine.

ndesanjo said...

Mkuu wa polisi anapoto tuhuma nzito namna hii, kuwa CUF ndio vinara wa ujambazi, lazima taifa lidai ushahidi. Mkapa alikaripia waandishi wa habari walipokuwa wakiandika kuwa nchi imejaa wala rushwa. Akataka waandishi watoe ushahidi.

Mahita katoa ushahidi wowote Miruko?

mark msaki said...

nimemjadili mahita bloguni mwangu. ndio maana sikumbakiza pale alipotajwa kama "mtu muhimu" na bwana michuzi. kwa kwa mara ya kwanza katika maisha yangu nimeona CV iliyoandikwa kama insha (ya huyu bwana). halafu ni mwanasiasa si polisi huyu hatufai aondoke! Ndesanjo, teyari nimeishajiunga na watanzania wengine kulaani kauli ya huyu bwana kuitikia wito wa bwana Lipumba...kutumia hiyo hiyo habari bloguni mwangu.. na kwenye www.cuftz.org section ya midahalo.

Reginald S. Miruko said...

Ndesanjo, Omari mahita Iddi hakutoa vielelezo vya CUF kujihusisha na ujambazi. Alivyodhani ni vilelezo vimepingwa na wananchi. Alitoa visu vyenye rangi ya nyeupe na nyekundu kuwa ni vya CUF (rangi ya bendera ya CUF). Kumbuka, visu hivyo aliwahi kuvionyesha Omari Mapuri wakati wa kampeni na Mahita akavionyesha kupitia ITV ya hapa siku moja ya uchaguzi, kuwa ni maandalizi ya CUF ya kuchafua amani ya TZ. watu wamehoji, je benki zinavamiwa kwa visu au Bunduki, je, kama mahita anawajua majambazi ni CUF, mbona hajawakamata? Mbona waliokamatwa na visu hivyo hawajafikishwa mahakamani? na mengine mengi...nakuachia mjadala.

Indya Nkya said...

Ndugu zangu ukweli ni kwamba jamaa anapindisha hoja. Ukiona mtu anashindwa kutoa maelezo yanayohusu fani yake na kukimbilia nje ya msitari huyu ni mtu hatari sana. mark wala huyu si mwanasiasa. Mwanasiasa gani anayeshindwa kushirikisha ubongo wake anapotoa maneno? Labda pengine tunatarajia makubwa toka kwa mtu mwenye uwezo mdogo sana

Jeff Msangi said...

Mimi naona ajiuzulu mara moja.Na kama anakaribia kustaafu hiyo isiwe sababu.JK sasa aache porojo,asije kuwa raisi wa porojo huku baadhi ya magazeti yakifagilia porojo.Hivi mpaka sasa JK kafanya nini zaidi ya maneno mengi na mikwara ambayo nahisi inaweza kuwa bubu?Anamuogopa Mahita?????

mark msaki said...

nimemuongelea kwa kirefu pale kwa Jeff alipochokoza kuhusu ripoti ya Jaji Kipenka!! kuna makala ya Mpinganjira nimeihusisha! Nkya ni kweli Omari anaweza kuwa na Mouth Diarhorrea....lakini alizidiwa kuona kuwa rushwa aliyoitoa haikutambulika vilivyo baada ya kuona nyangumi wenzie wana - shy away from him!! pale alipoonesha mabisu alikuwa anasema "I will spill the bins" kwa kiswahili ni nivunje kikombe nisivunje?? - na Kikwete alipotaja maeneo ya rushwa hapa mwisho alitaja RUSHWA YA SIASA!!kwa kweli mtihani JK anao na aujibu!

mark msaki said...

no alisema "I will spill the beans" - nitamwaga maharagwe - kwa kiswahili nivunje kikombe nisivunje? au kutia kitumbua mchanga!!

Post a Comment