Thursday, December 29, 2005

Kweli. Ni Lowassa


Kwa vyanzo vyangu vya uhakika nimetabiri Waziri Mkuu ni Edward Lowassa (pichani kulia). Sasa nathibitisha kweli ni yeye aliyeteuliwa na Rais Jakaya Kikwete (kushoto). Spika wa Bunge, Samwel Sitta, amemtangaza leo majira ya saa 11 jioni, aliposoma Barua ya Rais Jakaya Kikwete kutoka Ikulu ya Dar es Salaam. Wabunge, wengi wakiwa wa CCM walishangilia, ingawa wengi walidhani itakuwa hivyo kutokana na kile walichodai kuwa rafikiye wa karibu. Hiyo ndiyo timu ya wakuu wa nchi. Tusubiri tuone, je wataweza kutekeleza ahadi zao 143 kwa kasi mpya, ari na nguvu mpya? Kesho anaapishwa rasmi katika Ikulu ya Chamwino.

6 comments:

mark msaki said...

Tunashukuru kaka miruko,

nashukuru hawa radio maria

http://www.radiomariatanzania.co.tz/#

wananimegea live. sasa hivi ninamsikiliza mama makinda anajieleza na tunasubiri matokeo ya uchaguzi wa waziri mkuu.

cheers

mark msaki said...

kaka miruko,

tunaomba ukipata muda tulistie hizo ahadi 143 za ari mupya na kazi mupya na nguvu mupya

mwandani said...

hizi habari unazirusha kwa mwendo kasi kisawasawa toka hapo jikoni. Bora umerudi. Tumegee ahadi 143 tulio mbali nasi tuzijue.

Ndesanjo Macha said...

Hata mimi nina hamu na hizi ahadi 143.

mark msaki said...

jamni wanablogu kwanza nawatakia heri ya mwaka mpya!

jamani kuna kazi moja ya msingi. tuichambueni hotuba ya Kikwete bungeni! mie mpaka usawa huu nina wasiwasi kuwa kikwete anablogu!!tukutane kwenye blogu zenu kwa hili.

mie nitakuja baadaye kidogo na uchambuzi

cheers

Phabian said...

sawa kaka utabili wako si mchezo,ila wengi walitabili hivyo japokuwa sababu ya msingi ya uteuzi huu bado imejikita kwenye urafiki.Ngoja tuone kama sababu itakuwa utendaji wake au ni kweli urafiki.

Post a Comment