Saturday, December 24, 2005

Atafutaye Upata...upewa...ufunguliwa

kikweteKATIKA maisha haitakiwi kukata tamaa. Bidii na matumaini yanatakiwa ili kukuwezesha kupata kile ukitafutacho. Ndivyo ilivyokuwa kwa Bwana Jakaya Mrisho Kikwere, Rais wa nne wa Tanzania.
Yeye hakuchoka kuutafuta urais usiku na mchana, ni zaidi ya miaka 10, tangu aliposhindwa na Benjamin Mkapa (Rais Mstaafu) katika uchaguzi uliotajwa na wengi kwa ulikuwa wa 'mizengwe' (msamiati wa Kizanaki ukageuka Kiswahili). Tangia hapo mikakati yake iliendelea kwa muda wote, kwa kujijenga mwenyewe, kupambwa na vyombo vya habari, kuchangiwa fedha za kampeni na mengine mengi...ikiwa ni pamoja na kuwabomoa wote waliodhaniwa kuwa ni tishio la madaraka yake.
Yote hayo yamefanyika na matokeo yake yamekuwa mazuri, kwani amepata alichokuwa analilia. Mtoto akililia wembe mpe, ukimkata atajiju. Limebaki swali moja, je, Kikwete baada ya kupewa wembe atakata nini?

3 comments:

mwaipopo said...

Sina uhakika sana kuwa niko sahihi lakini Kiswahili changu kilichojeruhiwa na Kinyakyusa kinaniambia mzee ulisahau herufi 'h' kwenye taito ya stori hii. Hupewa, hupata na hufunguliwa.

Heri ya misa ya Kristu (Kristmas)

mark msaki said...

Miruko,

swali zuri sana na nategemea bwana michuzi kama tulivyomuomba amushauri mzee Kikwete kufungua blogu itakuwa ni jambo jema ili maswali haya akutane nayo huku huku.

ninachojua mimi kuhusu uongozi, wako watu wanaoupigania ili wawatumikie watu. wana charisma za uongozi, na wana nia dhabiti ya kusaidia watu na hivyo kuwa mashujaa kwa jamii wanayoiongoza.

kuna watu wanaupigania ili waweze tu kuwa na amri na kuwa wafalme. hawa hupigania kuwa watawala. hawana habari kabisa na kinachoendelea. bora tu wamekamata dola.

kuna wengine hupigania madaraka kwa kusukumwa na kundi la wateule ili walinde maslahi ya wateule yaliyoendelea kustawi miaka mingi baada ya uhuru na kuacha wengi kuwa masikini wa kutupwa.

sasa kwa hakika hakuna anayejua kuwa mheshimiwa wa sasa alipambana ikibidi kwa juhudi binafsi ili awe shujaa wa kukomboa watu, ili awe mtawala, au alinde wateule! Mungu ndio anajua!

cheers

Fikrathabiti said...

Ombi kama hilo kwa Meshimiwa kikwete nililitoa kwa wanablog wenzangu kumuomba MICHUZI afanye jitihada za kumpata waziri wa habari ajae na kumueleza kinagaubaga kuhusu nafasi ya blog katika harakati za kujikomboa kifikra na hatimaye kujiletea maendeleo.

Tukimpata huyo atakaekua kinara wa habari nadhani azma yetu ya kumuingiza bwana kikwete katika mtandao huo unaozidi kusumbua vichwa vya wengi kutafuta jina mbadala la kiswahili badala ya blog.

Post a Comment