Friday, November 11, 2005

Sanamu la Nyerere Hili Hapa, Je Wanafanana?

IMGP0015

7 comments:

Mija Shija Sayi said...

...kiasi cha mboga, lakini kichwani hasa zinapoanzia nywele mimi namuona mzee ruksa.

Indya Nkya said...

Vyvyote itakavyokuwa. Dola 200,000 zimeingia Korea. Zimeingia kukuza uchumi wa Wakorea. Sisi tutabaki na sanamu. Nyerere ni shule ya mawazo. Kumuenzi ni kutambua mchango wake wa mawazo na kuyafanyia kazi. Kuwa na sanamu haitoshi.

Boniphace Makene said...

Siku hizi kila kitu ni Nyerere, inaweza kuwa mradi mzuri huu, natambua wengi watabaki bumbuwazi kutojua kuwa inawezekana sana kumtumia Nyerere kufanikisha miradi ya Wajanja. Hizo gharama kwa ajili ya Sanamu, Je aliwahi kusema hili, mbona wakati akiishi hakujijengea kama tulivyowaona akina Sadam Hussein, kuna haja ya kufatilia tafakari ya hhoja ya Idya

mwandani said...

Naona anafanana zaidi na
Kim Il Sung.

Egidio Ndabagoye said...

Nilikuwa sifahanu Indya... dola 200000 kwa kumtengeneza Nyerere "feki"?

Ndesanjo Macha said...

Hivi Tanzania sanamu kama hiyo tumeshindwa kabisa kutengeneza miaka yote hii baada ya "uhuru"?

Nkya: kweli. Kumuenzi Nyerere sio kusambaza sanamu na picha zake na kuita majengo, viwanja na barabara jina lake...tunaweza kufanya haya yote. Ila huu sio msingi wa kumuenzi.
Mwandani: umenivunja mbavu...kumbe sanamu ya Kim II Sung hiyo?

Fikrathabiti said...

Big up brother NKYA!Unajua bwana tanzania ina ugua ugonjwa mmoja mbaya sana ambao kama hakuna jitihada za makusudi kutafuta tiba basi ujue utamaliza vizazi vyet vijavyo.

Hapa nazungumzia ugonjwa wa baadhi ya viongozi wetu kuogopa changamoto za kifikra na kujifanya wao kama wanajitosheleza kiakili na kimbinu walishanazo na wake zao pamoja na watoto wao.

Chuo kikuu cha Dar es salaam kuna chama cha wanafunzi wanaosoma sayansi ya siasa na utawala.Nilipokua kama mdau katika hicho kikundi tulikua na desturi za kuandaa mijadala mbalimbali kutafakari mustakabali wa nchi yetu bila nyerere na kutumia falsafa zake za maendeleo alizoziasisi miaka ya 60 lakini cha ajabu ni pale tulipotoa mualiko kwa viongozi wa serikali walikua hawaishi kutoa visingizio vya kuhudhuria.

Hakuna cha zaidi wanachoogopa zaidi ya changamoto zilizojaa muono mpana wa jinsi nchi inavyopaswa kuendesha kinyume na wao wafanyavyo.

Post a Comment