Sunday, October 02, 2005

Helkopter Itamsaidia Mbowe kuingia Ikulu?

Binafsi nilidhani ni jambo la kwaida. Sikuona ajabu pale Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilipotangaza kuwa kitatumia helkopta katika kampeni . Nimekuja kushangazwa na habari za gazeti moja kuwa ujio wa Helkopter ya iliyokodishwa Kenya kwa ajili ya kampeni, umebadili sura ya kampeni za Mgombea Urais wa Chadema, Freeman Mbowe. Habari zinasema kuwa mgombea huyo 'amepata mvuto wa ajabu na wa ghafla'. Watu wanamiminika kweli kweli katika mikutano yake. Wengine wanaacha mikutano ya wagombea wengine na kumfuata yeye. Naye amepata uwezo wa kuhutubia mikutano takriban 10 kwa siku, tena katika maeneo ya ndani ambapo wagombea wengine si rahisi kufika. (Picha ya mfano tu)

2 comments:

Anonymous said...

nimesoma hoja ya mbowe na helkopita.sikutaka kutoa maoni yangu kwa sasa hadi baada ya uchaguzi lakini kutokana na 'haja' yaani hoja ambazo naamini ni hafifu za baadhi ya wanaccm imebidi nivunje kimya changu.

nimesoma makala moja juzi katika gazeti la uhuru. mzee mmoja nayejiita mwasisi wa TANU akidai kuwa matumizi ya helkopita ni makubwa kuliko garama za uchaguzi. hii imeniudhi sana kwani ni upotoshaji wa makusudi wa ukweli wa mambo.hii si dhambi tu bali pia ni ukosefu wa hekima kama siyo busara.

anadai kuwa gharama za helkopita ni milioni takribani 200.je hii ndiyo zaidi ya gharama za uchaguzi?

anaongeza eti gharama hizo angetumia kwa ajili ya kujengea wananchi dispensari. sawa, lakini mbona hajawashauri CCM kufanya hivyo kwa kutumia pesa walizowekeza katika mradi wa kununua fulana, kozia, kukodi miziki na kubeba wananchi kuwaeta ktk miktano tena kwa lazima? je kwa nini hajaliona la gharama za shein, salma na kikwete ktk kampeni? je ana maanisha CHADEMA wasipe kampeni? kwa maslahi ya nani? kwa nini?

anaendelea kudai kuwa CHADEMA haina uwezo wa kufufua uchumi wetu, na badala yake CCM wanao huo uwezo! je nani aliuua huo uchumi? ni CHADEMA ambayo haikuwepo miaka 44 ya uhuu au CCM waliokaa madarakani muda wote tangu wakati wa baba yao TANU na ASP?

nadhani wakati umefika kwa watanzania kuwa makini na hawa wanaojiita wasisi wa tifa letu.maoni yao yapimwe kwa umakini, la sivyo tutaendelea na mahubiri ambapo
rais anaubiri, wabunge wanakariri, wasomi wanahariri bila kufikiri
taifa linasimama

Post a Comment