Thursday, September 22, 2005

Jamani, Acheni Kutuchekesha

Kichekesho. Kesi ya Nyani unampelekea ngedere! Hawa ni wapinzani wa Chama Tawala Tanzania kutoka vyama vya viasa 14, wasiopata ruzuku ya serikali, sijui kwa nini hawapati. CCM inapata sh 700 milioni kila mwezi, hawa hawapati hata senti moja, lakini wanashindana pamaoja katika uwanja mmoja, sina uhakika kama uwanja huu uko sawa . Sasa wamegundua kuwa wanazidiwa nguvu, wanalalamika kuwa hawawezi kuendelea na kampeni za kuingia Ikulu. Wamemwandikia Barua Rais Benjamin Mkapa, labda wamesahau kuwa Mkapa ni mwenyekiti wa Chama Tawala,CCM,na anataka CCM ishinde kwa kishindo cha Kimbunga cha Tsunami, Katrina na Rita. Ni kichekesho. Ndio maana kama ningekuwa mimi, ningesema Rais wa Nchi, kama vile Jaji Mkuu, Spika wa Bunge, wasiwe na vyama vya siasa. watapatikana vipi? Tuendelee kujadili.

No comments:

Post a Comment