Wednesday, October 12, 2005

Blogu zimeanza kuingiliwa na 'spams' kama e-mail?

Bila shaka wanablogu wenzangu mmeshakumbana na wachangiaji kwenye blogu wenye nia mbaya za ama kutangaza masuala yao ya ajabu ajabu au kutaka kusumbua wasomaji wazuri wa blogu. Mie yamenikuta. Nimekutana na matangazo ya casino na mitandao mingine ya ngono. Tusaidiane namna ya kuepukana nayo.

4 comments:

Martha Mtangoo said...

Haki ya Mungu yanayokusibu wewe nafikiri ndio yatakayotusibu wote kwa maana kwamba Mablogist ni kwamba tabia hiyo ni mbaya sana hata mimi minanichefua sana na walaaniwe, kama matangazo wanataka watangaze katika magazeti mbalimbali na siyo kutuchafulia mambo yetu. au siyo Dogo?

Indya Nkya said...

Msifungue katu asilani hivyo viuongo wanavyoweka. Mara nyingine wanakuwa wanakupeleka kwenye virusi vinavyoweza kuharibu kompyuta yako.

Rama Msangi said...

Yeah, dawa pekee kama alivyoshauri Idya ni kuacha kufungua viunganishi ambavyo unaona havieleweki eleweki kwasababu kurusi cha kutegeshwa kwa namna hiyo (iwe program au tangazo), huwa hakiwezi kufanya kazi hadi uwe umekifungua na ndio kinaleta madhara kwenye mashine yako. Kwa hiyo msivifungue.

Lakini ni tabia ya kukera sana na ambayo mimi ilinikumba mapema sana

Anonymous said...

unaweza kupunguza kasi ya hao ma'sperm' kwa kuweka uhakiki wa maneno katika dirisha la maoni. Hivyo mtu kabla ya kupandissha maoni inabidi ahakiki herufi. spam huwa zinatumwa kwa makundi. Maoni ya kweli hutumwa na mtu ambaye atahiyari kuhakiki herufi.

Tunga

Post a Comment