Tuesday, September 13, 2005

Mapuri anahitaji 'Mkakati'

Kama unafuatilia mambo hapa Bongo umeona jinsi Askari Magereza walivyowatandika Waandishi wa habari wawili na raia wengine na kuwajeruhi vibaya.
Lakini cha ajabu ni kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Omari Ramadhan Mapuri amebariki shambulio hilo na kulisifia kuwa: "Waandishi hao walistahili kuchapwa, kwani hawakuitwa katika eneo hilo na askari walikuwa katika operesheni. Wamiliki wa Vyombo vya habari nchini, kupitia chama chao, MOAT, wamelaani kitendo, wakamtaka Mapuri na Kamishana wa Magereza, Nicas Banzi wajiuzulu. Hilo halitoshi. Kama Mimi ningekuwa mshauri wao, ningependekeza vyombo vya habari vimsusie Mapuri na Wizara yake, walau kwa mwezi mmoja, isitoke habari hata moja kwenye vyombo vya habari inayohusiana na wizara hiyo hadi anyooke. Kila mmoja ana maoni yake. Nawasikiliza.

3 comments:

mwandani said...

Nafikiri inabidi Mapuri ashurutishwe kujiuzulu kwa kushabikia dhalimu zinazofanywa na askari dhidi ya watu wasio na silaha. Pili, waandishi wadai kulipwa fidia ya maumivu maungoni na kuzuiwa kutekeleza wajibu wao.

Indya Nkya said...

Pamoja na kususa mikutano yake na kutochapisha habari zinazohusu wizara yake, bado tunahitaji kujadili suala la majeshi yetu kujiona bora sana. Majeshi ya Tanzania yana mambo ya kusikitisha. Wao ni bora kuliko mwingine yeyote. Hili lisipoeleweka kwamba kuwa jeshini ni mgawanyo wa kazi tuu, bado wataendelea na huo upuuzi wa kumtandika kila mmoja.

Anonymous said...

Mkurugenzi!
Mh. Mapuri anahitaji mkakati wenye nguvu za tsunami. Kuna wakati huwa najiuliza kama Chama Cha Mapinduzi kinahitaji mtu kama Mh. Mapuri kuwa Katibu Mwenezi (Itikadi na Sera)! Na mtu huyohuyo kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani! Vyeo vyote viwili vinahitaji mtu makini, mwenye kutafakari kabla ya kuongea kama alivyofanya CP Adadi Rajabu. Lakini huwa najipa moyo kuwa watu kama hawa huja na huondoka kama walivyo watu kama CP Adadi Rajabu. Tofauti kubwa ni hisia za watu pale wanapoondoka katika nafasi zao...wengine hufanya sherehe mtu akibadilishwa au kutimuliwa kazi wakati wengie huhuzunika wanaposikia bosi wao anaondolewa! Akiondoka mheshimiwa Mapuri, wengi watafurahi...yeye atajisikiaje!!!?? Kwa mtu makini angeji-Iddi Simba au Aji-Mbilinyi!
Yetu macho na masikio. Naunga mkono wale waliosema hawana imani na tume iliyoundwa. Tuwaombee kina Mpoki na Kidanka...mapambano yaendelee.
OmeGa

Post a Comment