Tuesday, September 06, 2005

Vituko vya Lyatonga Mrema Havijaisha, Tazama hiki

AMA kweli mwenye macho ahambiwi tazama. Mwenye masikiniu ahambiwi sikia. Visa na vituko vya Mzee wa Kiraracha, 'Msomi' Augustine Lyatonga Mrema vinazidi kuzuka kila kukicha. Sasa ameibuka na kipya. Muda mfupi uliopita leo Sept 06 mjini Dodoma Mrema amezua jambo. Ni lipi? 'Alipomaliza kuhutubia mkutano wake wa kampeni, akatangaza kuwa kinachofuata, ni kwenda kushusha bendera ya Chama Tawala, CCM, na kupandisha ya Chama chake Tanzanaia Labour Party (TLP). Aliutaka umati wa washabiki umfuate kushuhudia tukio hilo la kihistoria. kweli walimfuata. Alianza kukata mitaa kutoka barabara moja hadi nyingine. Mwendo huo ulifiukia takriban kilometa 3. Wakati huo muziki mzito ulinguruma barabarani. wafuasi walikuwe wengi na ilikuwa kazi ngumu kwa Polisi kuwalinda, kwani maandamano hayakuwa kwenye ratiba ya mkutano huo. Hata hivyo, hakuna bendera ya CCM iliyoteremshwa na maandamano hayo ya hadaa yaliishia kwenye ofisi za TLP mkoa wa Dodoma'. Hiki ni kisa cha nne cha Mrema. Vingine ni vipi tangu mbio za urais zianze?
1. Alikwenda kuchukua fomu kwenye baiskeli ya magurudumu matatu
2. Alirudisha fomu akiongozwa na farasi
3.Alirudisha fomu akiwa amevaa joho, alilodai kavaa kwa kupata shahada ya kwanza (leo kasema alisomea Urais)

3 comments:

mwandani said...

inji yetu inataka kiongozi m-bunifu. Wallahi!

Martha Mtangoo said...

Haki ya Mungu yaani ni kaazi kwei kwei, Sauala la Mrema kufanya Vituko ni Ubunifu tu kwa maana katika kipindi hiki cha kampeni usipokuwa mbunifu utakuwa unafanya marudio!!!!!!!!

Anonymous said...

Audhu billillah, hima shetani rajimu, Mungu alipishilia mbali uchaguzi wa '95 ilikuwa almanusura tungeula wa chuya kwa sababu ya uvivu wa kuchambua. Huyu jamaa chizi yaani siyo chizi tu bali mgonjwa wazimu tena mgonjwa wazimu huyu ni mgonjwa wazimu maarifa. Dizaini zake kama Joji Bushi sema Joji Bushi ana kundi la wenye akili timamu kwa hiyo wanamshikia akili huyu Mrema hana wa kumshikia akili kwa hiyo anajiongoza mwenyewe.
Hiyo picha yake uliyoibandika hata kama hukusomea udaktari wa akili utaona sura ya mgonjwa wazimu. Lakini cha ajabu anajua kuwasambaratisha: kila chama anachopita anakiacha na maumivu. Halafu jinsi alivyokuwa smati hiki chama anachokiongoza sasa hivi kimemjengea nyumba kama walivyojengewa viongozi wengine wa chama tawala.
Huu wazimu wake tunaweza kuuita kwa maneno ya King Kiki ni "..kipaji alichopewa na Mwenyezi Mungu baba tangu akiwa tumboni kabla hajazaliwa.."

Post a Comment