Friday, September 02, 2005

Kwani lazima tupike kwenye mafiga?

Katika Uchaguzi Mkuu ujao, tutaona mambo mengi. Zitajitokeza kauli mbalimbali ambazo wahusika wanaita ni falsafa. Mimi sijui kama kweli ni falsafa. Mojawapo ni ile inayotumiwa na Jakaya Kikwete, mgombea Urais wa CCM. Ni ya 'mafiga matatu'. Kwamba ili utawala unoge lazima wananchi waichague CCM kwa mtindo wa mafiga matatu, yaani wamchague Rais wa CCM, Mbunge wa CCM na Diwani wa CCM. Kama hiyo itatekelezwa, ina maana Rais, wabunge na madiwani wote wataakuwa wa CCM. Mfumo wa Chama Kimoja utarejea kwa mlango wa nyuma. Lakini nionavyo mimi, si lazima kupikia kwenye mafiga matatu.
Wengine wanapika kwenye majiko ya umeme, gesi na mengine ambayo si lazima yawe na miguu nitatu. Hilo likifanyika bunge litachangamka, mabaraza ya madiwani yatachangamka na serikali itakayokuwa madarakani itawajibika kwa wananchi, kuliko kuchagua kwa mtindo wa Kizaramo wa mafiga matatu. Wengine mnasemaje.

1 comment:

msangimdogo said...

kauli mbiu yenyewe ni ya mafiga matatu unadhani kweli watakubali kushindwa kujinadi kwa staili hiyo hiyo ya mafiga matatu kaka??

Post a Comment