Tuesday, September 20, 2005

Alah, Kumbe Gaddafi 'Mzuri'!

GaddafiNakumbuka miaka ya 1978 na 1979 wakati wa vita kati ya Tanzania na Uganda. Rais wa Libya, Muammar Gaddafi aliisaidia sana Uganda ili iishinde Tanzania. Hakujali kuwa Dunia nzima ilikuwa imelaani vita hivyo. Alitoa askari wake wengi wakaingia vitani kumsaidia Iddi Amin Dada, lakini walifurumshwa na majeshi ya Tanzania na wengi wao walikamatwa matekwa. Sasa Gaddafi 'ameokoka' na kubadilika. Ameanza kuisadia Tanzania. Ametoa zaidi ya sh 6 bilioni kujenga msikiti mkubwa wa aina yake, utakaokuwa kama Taasisi ya elimu, dini na afya katika Mji Mkuu ulioshindikana wa Dodoma. Msikiti huo uliowekwa jiwe la msingi na Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein leo, umebatizwa jina la Gaddafi. Rais Benjamin Mkapa naye alishuhudia hafla hiyo. Msikiti huo utakuwa na uwezo wa kuchukua waumini 3,000 kwa wakati mmoja.

8 comments:

Indya Nkya said...

Hivi huo ndio msaada ambao watu wa Dodoma wanauhitaji kwa sasa? Labda ndio waliouomba kwake anyway!! Bilioni Sita Msikiti!!! Si masihara. Ni lazima watakaoswali huko wataenda peponi moja kwa moja (kama pepo yenyewe ipo). Lakini kuna atakayekwenda msikitini akiwa na njaa? Ataweza kweli zoezi zima la kuswali wakati tumbo likiwa wazi?

Mkina said...

Nani kakwambia kwamba Gaddafi kaokoa? Jua tu kwamba anahofia kifo na huenda anaona siku zake za kuishi zinakaribia ndiyo maama nadhani kujenga misikiti, kuusimaia kidete umoja wa Afrika ndiyo njia salama aidi ya kumuepusha na janga la moto siku ya kiama (kama ipo)

Indya Nkya said...

Nadhani kajenga misikiti kufuatia maombi aliyopata toka kwa wahusika. Pengine angeombwa msaada wa kufanya jambo jingine angefanya kama msaada wake haukuwa na masharti kama ya IMF na WB au wahisani wengine.

Martha Mtangoo said...

Tehe tehe, kwa kweli kila chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho unajua hata mimi nahofia kuwa Mshkaji wangu Ghadafi anahofia kufa na anatambua siku zake za kuishi hapa duniani zibebaki chache sana ili angalau ajaribu kumridhisha Mungu inabidi afanye hivyo, any way tumpe Mwaka mmoja wa kuishi hapa duniani tuone atakuwa amesaidi vitu gani katika Misikiti na Masinagogi!!!!!!!!1

Rama Msangi said...

kulikuwa na nadhani haka kautamaduni badfo kapo wanakaita kakusafisha fedha chafu, nadhani unakaelewa na kwahakika ukitizama kwa undani utabaini kuwa wengi wa jamaa wanaojiita watoa misaada iwe ya masharti au laa ni wale ambao walishiriki katika kutenda uhalifu wa hali ya juu. Ndio, kwani hatuoni jinsi majambazi wanavyokimbilia kuwa walokole na kujenga makanisa na hata hii misikiti?, ndio maana hata wanaoomba humo dua zao ni vigumu kusikilizwa kwasababu majengo hayo yamejengwa kwa fedha zinazonuka damu na dhuluma na kibaya zaidi wanajua hilo hao wenye kuyatumia majengo hayo.

lakini anyway, let them do their best and God can do the rest

Anonymous said...

Mgogo maskini ya Mungu ni jalala. Kila kitu natupiwa yeye: Ujenzi wa makao makuu ya Chama cha Mapinduzi na makao makuu ya serikali ya Jamhuri ya Muungano alipelekewa bila masharti, jengo la pili la Bunge, kiwanda cha mivinyo, na sasa anapelekewa Mungu. Tatizo sijui ni la watu wa Dodoma au wawekezaji wa haya masuala kwa sababu hivi vitu vyote vingepelekwa kwingine ungeona mabadiliko ya watu wa sehemu hiyo lakini aliyewahi kufika Dodoma miaka ishirini iliyopita na akafika tena leo atawakuta watu wa Dodoma wapo vile vile. Labda safari hii kwa huu msikiti tunaweza kuona mabadiliko ya majina ya mwanzo Mohamed Matonya, Mwajuma Madeje, na mengineyo. Halafu makanzu na balaghashia kwa wingi badala ya lubega.
Salamu aleikhuim Dodoma!
Fidelis Tungaraza, Helsinki, Finland.

Anonymous said...

Wasalaam!

Watanzania kwa kupenda mambo ya chee, yani vya kupewa bure tumezidi. Sijui ni nani asiyejua habari za huyu Gadafi, hata mtoto mdogo ukimtajia anaweza kukimbia avunjike mguu. Hiyo ndo gear ya kuingia Tanzania kama hamjaelewa, na hivi skendo zake zilivyo mbovu, nachelea kusema neno ila huo msaada iko siku kama si kwa neema ya Mungu atuepushie mbali; utatokea watu puani. Tena bila hata kufikiri kweli unapewa jina lake?? jamani watanzania hebu amkeni na kuangalia mbele maana huko tunakopelekwa ........ sijui

Mungu nakusihi utuponye na mkono wa adui., Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Dunia. Amina

Nemy -

mloyi said...

Kubalini anachokupeni, kwenye mahojiano na SABC AFRICA kule Johanesburg alisema njia pekee ya ukombozi wa waafrika ni kufuata uislamu, sasa naona anatuletea ukombozi. Kauli yake ilinidhoofisha, niliiona kama njia nyingine ya kuvunja umoja uliokuwa unaanza kuchomoza. Sijui kama alifikiria kwamba kuna wenye dini zao wanazozilinda kuliko yeye anavyolinda yake au kufikiria wasiokubaliana na hizo dini pekee?

Post a Comment