Wednesday, August 03, 2005

NVUVU YA VIJANA CCM YAWATISHA WAZEE

ILE inayodaiwa kuwa ni falsafa ya Nguvu mpya, Ari mpya na Kasi mpya ya Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama Tawala, CCM, Jakaya Kikwete, imewatisha wazee wengi. Vijana nchi nzima wamezizima na kutaka kuwang'oa wazee kwa nguvu zote. Majimbo mengi yamevamiwa na vijana wakidai kuwa ndio wenye uwezo sasa wa kuwa wabunge. Lakini sidhani kama nguvu hizo zitashinda takrima. Ngoja tuone mwisho wake. Nitaendelea kukuletea.

1 comment:

Ndesanjo Macha said...

Umegusia jambo muhimu sana. Mtu akija na kauli mbiu ya "vijana, vijana..." na mzee akaja na mikono mfukoni na takrima...nani atashindana naye? Wazee hawa eti wanadai kuwa takrima ni sehemu ya utamaduni wetu..eti ni ukarimu wa kitanzania. Huo ukarimu wa mara moja kila baada ya miaka mitano sidhani kama ni sehemu ya utamaduni wanaozungumzia.

Post a Comment