Tuesday, July 12, 2005

Hayo yalikuwa ya Musa, sasa haya ya Firauni

Kumbe usichokijua ni sawa na usiku wa giza, lazima uwe kama paka ili uweze kuona vizuri.
Wakati mimi nikishangaa kuona watu wanakula kweleakwelea, kumbe kuna watu wanakula vitu ambavyo mimi naviita vya ajabu zaidi. Watu mbalimbali wameleta maoni yao, ebu yasoma haya kutoka Morogoro:

Twaha O Kivale anasema,

"Tembea uone mambo na kama hujaumbika basi huwezi kufa na ukifa ukiwa na matendo mazuri unaweza kuingia kwenye bustani ya Adam na Hawa kwa matendo yako mazuri tu. Hivyo ndivyo Mungu anavyo taka na ndio maana vyakula tunavyokula vinafanana kabisa na kama vinapishana basi ni kwa asilimia kidogo sana.
Kwangu mimi sioni ajabu kwa watu wa Kondoa kula hivyo vindege kwani hata kwetu Morogoro katika wilaya za Kilombero na Mahenge ni kitu cha kawaida kabisa na vinapatikana kwa mtego unaotengenezwa kienyeji uitwao kijaka lakini kama ilivyokawaida ya mkoa huu wa Morogoro hususani wilaya hizi huwa hawana tabia ya kuuza hata mazao ya matunda kwa kipindi kirefu huko vyuma na hupenda sana kuvua samaki na samaki hao kuna aina nyingine ya samaki hawana tofauti kabisa na nyoka ambao wanakula wachina huitwa Mkunga kwa hiyo karibu kwetu Ifakara upate kula kitu kingine kinaitwa ngopango hana tofauti na mdudu aitwaye vunjajungu.

Wengine mnasemaje, wenzenu wanakula hata vunjajungu!

No comments:

Post a Comment