Friday, July 08, 2005

Unajua kuwa Kweleakwelea Wanaliwa Dodoma?

*Ni ndege wadogo wanaoshambulia mazao
*Walaji wake wameongezeka
*Mmoja adai ni watamu kwa ugali

Na Reginald Simon, Dodoma

KITU ambacho unakula hakiwezi kukutia kinyaa, lakini mwenzako asiyekula kitu hicho anapata kinyaa. Mfano, hapa Tanzania makabila mengi yanatumia wadudu aina ya kumbikumbi, lakini hawezi kutumia senene kama wenyeji wa mkoa wa Kagera wafanyavyo. Senene zinawatia kinyaa. Kitu kipya nilichoona hapa Dodoma ni ulaji wa ndege wadogo aina ya kweleakwelea wanaoshambulia mazao. Pengine hiyo ni namna ya wenyeji wa Wilaya ya Kondoa, Warangi, kula ndege hao ili kuwamaliza wasiendelee kushambulia uwele na mtama wao. Masuala ya vyakula yana historia ndefu, pengine, Adam na Hawa (Eva) kama wangekuwa Wachina, watu wote tungekuwa tunaendelea kuishi katika Bustani ya Eden kwani, badala ya kula lile Tunda la Katikati na kumchukiza Mungu, wangekula yule nyoka aliyewadanganya.

4 comments:

ARUPA said...

Ni kweli kama Adamu na Eva wangekuwa wachina tusingekuwa na Dhambi na tungeishi Edeni, lakini ina maana ulikuwa hujui kama kweleakwelea ni ndege kama ndege wengine ambao hata wewe huwala?

Kwa taarifa yako kwelea kwelea ni watamu sana kama njiwa poli, hivyo usiwaonee kinyaa jaribu kuojna siku moja.

Anonymous said...

Nakubaliana na wewe Mkurugenzi ingawa nina wasiwasi kidogo. Inawezekana wenyeji wako Warangi wakawa wanawala kweleakwelea kwa sababu ya njaa na/au dhiki. Uwele au mtama wao kikawa kisingizio cha watu kama nyie kujenga hoja. Ukikubaliana na mimi, tupange mikakati ya kuwasaidia.
Hata hivyo, hongera kwa kutuhabarisha.

Anonymous said...

Tembea uone mambo nakama hujaumbika basi huwezi kufa na ukifa ukiwa na matendo mazuri unaweza kuingia kwenye bustani ya Adam na Hawa kwa matendo yako mazuri tu.hivyo ndivyo mungu anavyo taka na ndio maana vyakula tunavyo kula vinafanana kabisa na kama vinapishana basi ni kwa asilimia kidogo sana kwangu mimi sioni ajabu kwa watu wa Kondoa kula hivyo vindege kwani hata kwetu morogoro katika wilaya za kilombero na mahenge ni kitu cha kawaida kabisa na vina patikana kwa mtego unao tengenezwa kienyeji uitwao kijaka lakini kama ilivyo kawaida ya mkoa huu wa morogoro hususani wilaya hizi huwa hawanatabia ya kuuza hata mazao ya matunda kwa kipindi kilefu huko vyuma na hupenda sana kuvua samaki na samakihao kunaaina nyingine ya samaki hawana tofauti kabisa na nyoka ambao wanakula wachina huitwa Mkunga kwahiyo karibu kwetu ifakara upate kula kitu kingine kinaitwa ngopango hana tofauti nma mdudu aitwaye vunjajungu.

Martha Mtangoo said...

E Bwaan EE ni Kweli Adamu na Eva Wangekuwa Wachina Ingekuwa safi sana maana badala ya kula Tunda Wangemla yule Nyoka, Ni hivi Kweleakwelea ni Kama Kuku tu Si unajua tena Kuku ni Ndege? kwa hiyo wala isikupe shida sana ukitaka kujua uhondo wa Ngoma Ingia Ucheze na ukitaka kujua utamu wa Kweleakwelea Onja kamwe hutoacha. lakini kinachowafanya Ndugu zangu warangi kula hao ndege saaana ni kwa ajili ya kuwapunguza wasile mazao si unajua tena Dogo ukisubiria mpaka watu wa Kilimo waje kuwamaliza itakuwa kazi ngumu sasa ili kuwapunguza inabidi wafanya hivyo, Keep intouch Cheers

Post a Comment