Monday, July 25, 2005

UBUNGE NI ULAJI, Kweli?

Si wote wenye utashi na uwezo wa kunena haya. Ni wachache. Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe,amesema waziwazi kwenye mkutano wa hadhara mjini Songea, Ruvuma kuwa 'Ubunge ni Ulaji Mtupu'. Anamaanisha nini? Eti mbunge akimaliza muda wake wa miaka mitano anakabidhiwa kitita cha sh 34 milioni, ambazo mfanyakazi wa kada nyingine hapa nchini hawezi kupata kwa maisha yake yote ya kazini. Kama amenukaririwa vizuri, ameongeza kuwa kila mwezi, kila mbunge anapewa posho ya Jimbo sh 1 milioni. Faida nyingine hatuzijui, lakini wakati wa vikao vya Kamati na Bunge lenyewe hupata posho isiyopungua sh 80,000 kila siku. Yawezekana si nyingi kutokana na kazi zao, lakini Mbowe ambaye ametangaza hagombei tena amesema ni Ulaji Mtupu! Anasema hawezi kuendeleza ulaji huu na kuwa wengi wanaotaka ubunge si kutaka kusaidia wananchi bali kwa maslahi binafsi.
Mbowe huyu huyu sasa anataka kuwani Urais, atadhibiti vipi huu ulaji?

No comments:

Post a Comment