Rais Mstaafu wa Marekani Bill Clinton wiki iliyopita alizindua asasi ya Rais Mkapa ya Kupambana na Ukimwi. Akiwa na mwenyeji Rais Mstafu Mtarajiwa wa Tanzania, Clinton walipata fursa ya kuzungumza kwa undani, kama picha hii ya Ramadhan Kinyonya wa Business Times inavyoonyesha. Mazungumzo yao yalikuwa hivi:
BILL: "Unajua William inabidi uwe na mkakati wa kukuondolea umasikini baada ya kipindi chako cha Urais, naona hapa umecheza kama Pele. Usipojiangalia mapema utaishi kwa tabu sana baadaye."
WILLIAM: "Unadhani mi mjinga, haya niliyajua tangu muda mrefu. Wife alianzisha NGO yake kubwa ya kitaifa, Equal Opportunity Trust Fund (EOTF), lakini juzi juzi tu wabunge kule Dodoma wameanza kuchonga, eti EOTF irudishwe serikalini na kuendeshwa na Ma-First Lady wote wajao. Wivu tu! Hapo nikaona niwahi nitoke na hii ya ukimwi"
BILL: "Hiyo safi hata mimi ninayo kule kwangu na inapata misaada mingi, wewe mwenyewe ni shahidi, maana kutokana na mapesa hayo nimeimegea nchi yako kiasi fulani kununulia dawa za Ukimwi" Unajua...
WILLIAM: Chuna Bill, naona huyu mpigapicha anatusikiliza.
BILL: Poa tutaongea baadaye.
Je unadhani walizungumza nini baada ya mpigapicha kuondoka?
2 comments:
Kaka hapa naona umeamua kuingia deep vilivyo. Ni ubunifu mzuri sna huu. Nani anataka kustaafu kifala bwana. Hivi EOTF ni ya Anna Mkapa na si ya First ladies wote? Ina maana kila first lady ataanzisha ya kwake basi!!
Wewe kijana, naona sasa umenza kuwa na akili, jitahidi. Nakuandalia nafasi ya uhariri kwenye gazeti langu. Hiyo ya kuteta kwa waheshimiwa hao ni safi mno na huenda ikwa wa kweli, si ulikuwepo au ulikuwa umepenyeza kinasa sauti chako kwenye soksi za Billy. Mie bado nachechemea, jamaa wa al-Qaeda bado wameniteka. Nimefungwa mikono na miguu, hapa naandikia ulimi, kazi kweli kweli.
Kwelea kwelea vipi, nyama yao tamu au namna gani, jamaa wamesema umeionja eti ni zaidi ya senene.
Post a Comment