Monday, July 18, 2005

Hawa 500 wanyongwe hadi wafe!

Takwimu za karibuni kabisa zinaonyesha kuwa Tanzania ina watu 500, waliohukumia adhabu ya kifo walioko magerezani, wakisubiri utekelezaji wa hukumu yao. lakini hiyo siku inayosubiriwa haiji. Kila mlango wa gereza ukifungul.iwa wanadhani siku yao imewadia, lakini wapi! Siku haifiki.
Kisa? Rais Mkapa anaogopa kumwaga wino ili watu hao wanyongwe.
Pia, Rais ana kigugumizi cha kuwabadilishia adhabu ili walau wafungwe maisha. Yote ni yale yale: Hatutawaona tena.
Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ilipotembelea Gereza la Ukonda, Dar es Salaam, wafungwa hao waliwaeleza wajumbe: "Mnatutazama nini, mwambieni Rais atunyonge"
Mbunge wa Njombe Kaskazini (CCM), Jackson Makwetta, alisema bungeni hivi karibuni: "Kwa nini Rais atekelezi hiyo sheria ya kuwanyonga watu hao 500? Kama Haitekelezeki utawala bora uko wapi?"
Watu wa Haki za Binadamu, wanasema adhabu ya kifo haifai kwani inaondoa uhai wa mtu mwenye haki ya kushi, inamnyima mhusika nafasi ya kujirekebisha, na kuwa kama kuua ni vibaya kwanini hawa wahukumiwe kufa?
Baadhi ya wanajamii na Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Andrew Chenge: Sheria bado inafaa, wengi wanadhani adhabu inayostahili kwa aliyeua ni kuuawa. WEENGINE MNASEMAJE?

1 comment:

Indya Nkya said...

Kuna sahihi za vifo zinatiwa kila siku. Watu kwa makumi kila siku wanauawa kwa magonjwa yanoyotibika kama Malaria na kipindupindu kutokana na sera mbovu. Hizo si hukumu za vifo au kwa kuwa hazijatolewa na Jaji?

Post a Comment