Tanzania inaingia katika ngwe ya tatu ya uchaguzi tangu mfumo wa vyama vingi uanze kutumika hapa, mwaka 1995. Mara mbili mfululizo, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa kinashinda, tena kwa kura nyingi (Hata kama wengine wanasema za wizi).
Wapo 'wana-SIHASA' hususan wenyeviti wa vyama vya Upinzania wanaodhani kuwa wenyewe pekee, si mtu mwingine kwenye vyama vyao, ndio wanaofaa kuwa wagombea. Waligombea mara ya kwanza wakashindwa. Wakarudia tena wakashindwa vile vile, tena mara hii vibaya zaidi. Sasa hawajachoka wanaingia tena Mwaka huu na fomu wameshachukua. Tuone itakavyokuwa.
Hawa ni Kina Augustine Mrema (TLP), Profesa Ibrahim Lipumba (CUF) na John Cheyo (UDP) ambao wanataka kuonekana kama wagombea Urais wa maisha. Je, hiyo inakubalika? Vyama vyao havina vijana au watu wengine wapya? Kazi kwenu wapiga kura.
No comments:
Post a Comment