Saturday, June 25, 2005

Mbunge Mwingine afariki

Mbunge atutoka Huyu ni Margareth Bwana, Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) alifariki jana, kutokana na Ugonjwa wa Moyo. Mbunge huyu anafanya wabunge waliokwishafariki katika bunge la Awamu ya Nne kuwa saba. Wengine ni Abu Kiwanga (Kilombero), Comrade Thadeus Kasapira (Ulanga Mashariki), Yete Mwalyego (Mbeya Vijijini), Sebastian Kinyondo (Bukoba Vijijini),Hassan Diria (raha Leo) na Frank Michael Mussati (Kasulu Mashariki). Majimbo yote hayo, isipokuwa Bukoba Vijijini yako wazi kwa kuwa sheria hairuhusu kufanya uchaguzi ndani ya mwaka wa uchaguzi.

No comments:

Post a Comment