Saturday, May 21, 2005

Ni Maelewano wa Kweli au Danganya Toto ya Mrema

Katika Historia ya vyama vingi Tanzania, juzi Augustine Lyatonga Mrema, yule mpinzania wa Tanzania bingwa wa migogoro alitangaza kuachana na migogoro kabisa. Pengine kubwa kuliko yote ni uamuzi wake wa kutangaza kitu alichoita 'Amnesty' Kwamba ni upatanisho wa Tanzania Labour Party (TLP) kwa wanachama aliowatimua katika chama. baadhi yao wamepewa madaraka waliyokuwa nayo. baadhi tu ni Muasisi wa TLP, Leo Herman Lwekamwa, Katibu Mkuu wa zamani, Harold Jafu na Katibu Mwenezi, Thomas Ngawaiya. Kama Mimi nilivyo na wasiwasi hata waliosamehewa pia wanawasiwasi Soma hapa uone. Labda ni kweli, ukizingatia kuwa Mrema amerejeshewa mamilioni ya Ruzuku, sh milioni 42 kila mwezi kama NIpashe inavyosema kuwa sasa TLP ngangari

No comments:

Post a Comment