Monday, April 25, 2005

Hivi lazima mgombea achafuliwe?

Kupakana matope, matusi, tuhuma hewa na mambo mengine unayoweza kuita machafu ndiyo yanayotokea tanzania kwa sasa. KIla mgombea anasemwa lake, wengine wanakanusha na wengine wanauchuna. Kakini kama tujuavyo, uongo ukisemwa sana hugeuka ukweli, hivyo kukanusha ni muhimu.
Ukabila, ukanda, rangi ya mtu na asili yake ni mambo yanayojitokeza sasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi ndani ya Chama kinachotarajiwa kuendelea kutawala, CCM. Badala ya kujadili hoja, tunajadili majungu kwa nia ya kumkweza mgombea 'wetu' kipenzi cha watu. Hebu soma hii uone yanayojiri.
Wengine wameitwa wala rushwa, uthibitisho umekosekana, mwingine eti mzee sana, lakini anaandamwa yeye peke yake na mwingine mwenye umri sawa hakuna anayemzungumzia kwa kuwa si mshindani mwenye nguvu. Ingawa logic haisemi hivyo, lakini, mbona Joseph Ratzinger (78) amechaguliwa kuwa Papa licha ya umri wake mkubwa...Mkomeni Malecela 'wetu' Urais si kubeba zege bwana!

No comments:

Post a Comment