Wednesday, January 12, 2005

Uhuru wa Habari muhimu kama Uhuru wa Kuabudu

NIMEAMUA. Kuamua ani kuamua tu, hata kama unachoamua ni kichekesho. Lakini mwenye busara anatarajiwa aamue jambo ambalo ni jema, na maana (si kichekesho). Nimeamua nini? Nilichoamua leo ni kuungana na wenzangu duaniani kote, kama wanavyofanya watu wa misa, kutetea uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania na ulimwenguni kote. wakati natembea ndani ya blogu mbalimbali, nilikutana na blogu ya Mtanzania anayeishi marekani, Ndesanjo akiwa amechapisha kitabu cha Mwembechai, ambacho serikali ya Tanzania imekataa katakata kisiwafikie wasomaji. Nilifarijika na kuamua kuanzia hapo kazi yangu ya kupambana na minyororo ya uhuru wa habari.

No comments:

Post a Comment