Monday, January 10, 2005

Umasikini, maradhi na vita ndo Tsunami ya Afrika?

Janga kubwa duaniani katika kipindi cha karibuni ni Tsunami, tetemeko la chini ya bahari lilioteketeza maisha ya zaidi ya watu 150,000. Hilo tumelishabikia na vyombo vya habari vimelionyesha kwa kila aina ya mbwembwe. Lakini, tukumbuke pia kuwa hapa Afrika idadi kubwa ya watu zaidi ya hao wanateketea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, na wakubwa wanaendelea kusambaza silaha ili tumalizake. Pia umasikini na maradhi kama ukimwi, kipindupindu na baba yao malaria, yanazidi kutumaliza. Tusipigane na janga moja, yanayotumaliza ni mengi.

1 comment:

Mkina said...

Kwanza heri ya mwaka mpya...naona mambo yako yatakuwa makubwa sana mwaka huu mpya na pia nakushauri tu ndugu yangu...sasa upasuaji kichwa acha...umekuwa mkubwa miaka 40! kah.
Nimekuona nawe umejiunga na chama chetu cha blogging...karibu sana na naomba mara kwa mara upate ushauri kwangu kama unakwama na kwa taarifa yako tunaanzaisha chama kabisa cha bloggers. kaa mkao wa kula...kuna mambo mazuri yanakuja..jitahidi.
Hivi nami umeniona ama unaingia tu bila kujua baba zako wamo...mtoto utapata laana bure.Tuwasiliane Pasua kichwa.
Nasikia unataka Ubunge...wa wapi...haya shauri yako bwana majimbo hayo yana wenyewe subiri mapya kama unajipenda unataka watu wache fedha zenye sura zai na wake zao...ohhhh
Pata mtazamo mpya kwenye blog hii: www.mkina.blogspot.com

Post a Comment