Monday, April 02, 2012

Wasemavyo CCM Kuhusu Ushindi Arumeru

Mshindi wa kiti cha ubunge, Joshua Nassari


"Mwigulu Nchemba


HONGERA CHADEMA, HONGERA MHE JOSHUA NASARI MB ARUMERU MASHARIKI CHAGUO LA WAMERU. KWA NIABA YA TIMU YA KAMPENI YA CCM NAKUPONGEZA KWA RIDHAA ULIOPEWA NA WANAARUMERU."

"Nape Nnauye

Hongereni watani (Chadema) kwa ushindi Arumeru Mashariki. Ninawapongeza mmeshinda! Ndio kauli ya wana Arumeru Mashariki nasi tunaiheshimu! Fanyeni kazi kutimiza mliyowaahidi wapiga kura. Kila lakheri! (facebook)

Chama Cha Mapinduzi, kimeyapokea matokeo ya kura zilizopigwa na kutangazwa na tume ya Taifa ya uchaguzi kwa chaguzi ndogo zote, ule wa Arumeru Mashariki na zile za kata nane zilizofanyika jana nchini kwenye maeneo husika.

Kwa heshima nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati watani zetu, CHADEMA kwa ushindi walioupata Arumeru Mashariki na kwenye kata tatu(Kirumba, Kiwira na Lizabon). Lakini pia nawapongeza CUF kwa kushinda ile kata ya Tanga. Katika kata nane zilizokuwa zikifanya uchaguzi CCM tumeshinda kata nne. Tunawashukuru wananchi kule walikoendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kata hizo nne. TUNAWAAHIDI KUWATUMIKIENI KWA MOYO WOTE.

Matokeo ya kura hizi kwa ujumla yameonyesha sauti ya wapiga kura kwenye maeneo husika, ndo maana tunaheshimu maamuzi yao. Tunatoa wito kwa vyama vilivyoshinda kwenye maeneo hayo kuhakikisha vinatumia muda na dhamana waliyopewa kutekeleza yale waliyowaahidi wapiga kura wao.

CCM tutatumia matokeo haya kufanya tathimini ya kina na kuangalia wapi tuliteleza ili tufanye marekebisho kuhakikisha makosa hayarudiwi tena. Kimsingi uchaguzi huu umeisha na tufunge mjadala wa uchaguzi tujikite katika kuwaletea maendeleo wale waliotuchagua.

Nawatakieni kila lakheri wote mliochaguliwa, nawatakieni utumishi uliotukakuka!
" (Jamiiforum)


"John Chiligati

HONGERENI CHADEMA KWA USHINDI WA ARUMERU MASHARIKI,DEMOKRASIA IMECHUKUA MKONDO WAKE,HONGERENI SANA CCM KWA KUONYESHA UKOMAVU WA KISIASA KWA KUYAKUBALI MATOKE NA KULINDA AMANI CHINI YA DEMOKRASIA CHANGA,TUJIPANGE,TUNA NAFASI YA KURUDISHA IMANI YA CHAMA CHETU KWA WATANZANIA"

No comments:

Post a Comment