Tuesday, October 25, 2011

Kwa nini Dk. Shein kachelewa kuingia Baraza la Mawaziri?

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohammed Chande Othman, kuwa mjumbe na kushiriki katika vikao vya Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kifungu namba C ibara ya kwanza ambayo inawataja wajumbe wa Baraza la Mawaziri kuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Mawaziri wote.

Swali ni je, kwa nini alichelewa kuapishwa na kuingia kwenye baraza tangu alipochaguliwa mwaka jana, na baraza lilikuwa likutana mara kwa mara akwa shughuli mbalimbali? (iliwahi kuelezwa kuwa hata karume alikuwa haiingii kwenye vikao vya baraza). Pia kwa kuwa anaapishwa na Jaji Mkuu, kwa nini asiende Mahakama Kuu au ya rufaa kuapa, bali iwe Ikulu kwenye mhimili mwingine?

No comments:

Post a Comment