"Those who are too smart to engage in politics are punished by being governed by those who are dumber."-Plato
Sunday, October 02, 2011
Kampeni Igunga zamalizika kama sinema
Na Benjamin Masese, Igunga
KATIKA hali isiyo ya kawaida mgombea wa chama cha Wananchi (CUF) Bw. Leopold Mahona
amejikuta akirushana ngumi na askari polisi baada ya kushushwa jukwaani kutokana na
kuvamia mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Lengo la kuwarushia polisi ngumi ni kutaka kuwatoroka na kwenda kupigana na Mbunge
wa Biharamulo, Dkt. Anton Mbasa aliyefika hapo na kuamuru polisi kuwashusha jukwaani kwa
kuwa muda wao ulikuwa umeisha, na Chadema ndicho kilitakiwa kuhurubiwa mkutano.
Kutokana na hali hiyo mbunge wa viti maalum CUF mkoa wa Tabora Bi. Magdelena Sakaya
aliingilia kati na kurusha ngumi ovyo hovyo akipambana na wafuasi wa Chadema
waliokuwa wakiwasadia polisi kuwaondoa jukwaani na kuwaingiza ndani ya ndege yao
yenye namba 5Y-BTW.
Pia Manaibu Katibu Mkuu wa CUF, Bw.Ismail Jusa (Zanziba) pamoja na Bw Julius Mtatiro
(Bara) walishindwa kuvumilia na kuingilia kati kitendo kilichosabaisha uwanja mzima
kuwa mtafaruku.
Kwa mujibu wa ratiba ya tume ya Uchaguzi ilionesha kuwa CUF walitakuwa kufanya
mkutano wao Kata ya Nyandekwa kuanzia saa 3.00 hadi 4.30 asubuhi katika uwanja wa
shule ya msingi Nyandekwa lakini hawakufika muda huo.
Ambapo Chadema ilitakiwa kufanya mkutano wake eneo la Mbuyuni kiwanja cha Sungusungu
kilichopo mita 100 kutoka Cuf walipokuwa wanafanya mkutano wao.
Kutokana na tukio polisi waliokuwa wamekaa ndani ya gari lao walilazimika kusaidia
ili kutuliza ghasia hiyo kwa kuwashika Bw. Mahona na Bw. Mbasa.
Mbali ya askari hao kumuzuia Bw. Mahona alionekana kuwazidi nguvu kwani alikuwa
akirusha ngumi na kuwasukuma na kupepesuka na kumuacha lakini kutokana na watu
waliokuwepo waliweza kumshawishi na kumtuliza na kumuingiza ndani ya ndege.
Akizungumzia sakata hilo Bw. Mbasa alisema amesikitishwa na kitendo cha CUF kuvamia
mkutano wao kwani wamekiuka sheria na ratiba ya Tume ya Uchaguzi iliyopangwa.
Alisema kuwa imedhirisha wazi CUF waliagizwa na CCM kwani wafuasi wa chama hicho
walionekana maeneo hayo kuwasaidia lakini hawakuweza.
"CUF wamebipu na sisi chadema tuna salio la kutosha hivyo tumewapigia,"alisema Mbasa.
Naye Katibu Mkuu wa Chadema Dkt. Willibrod Slaa alisema amelaani kitendo hicho na
kusema hiyo dalili za kushindwa hivyo wanatafuta kisingizio cha kutaka kuituhumu
Chadema.
No comments:
Post a Comment