Picha hii niliipiga asubuhi Julai 15, 2007 katika Hotel ya Kobo Palace Arusha.
Nilimfuata Danny Mwakiteleko nikamwomba anipige picha ya kumbukumbu kwa kutumia kamera yangu. Alipomaliza, nami nikamtwanga moja. Sikujua, kumbe alikuwa ananiachia kumbukumbu ya milele.
Mwakiteleko alipata ajali ikiwa ni siku tatu tu tangu turejee kutoka Arusha kwenye mkutano wa Wahariri, uliojadili 'Responsible Journalism'.
Gari alilokuwa akiendesha (picha ya chini) niliingia kwenye uvungu wa lori katika eneo la TIOT, Tabata usikuwa wakati akitoka kazini. Aliumia vibaya kichwani. Alikimbizwa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na kufanyiwa upasuaji wa kichwa, lakini mapenzi ya Mungu kwake yalikuwa makubwa kuliko ya yetu sisi.
Ilipofika Julai 23 saa 10 alfajiri Mungu alimuita, naye akaitikia. Aliagwa jana nyumbani kwake Tabata, Dar; Atazikwa leo Mbeya. Hatutamuona tena Danny. Kwaheri Danny Mwakiteleko, ulale pema Kamanda. Tuandalie nafasi maana nasi tutafuata.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe. Amen
No comments:
Post a Comment