Monday, November 15, 2010

CHADEMA ashinda Mpanda Mjini, CCM Mpanda Vijijini

Mbunge Mteule wa Mpanda Mjini, Said Amour Arfi (pichani) amefanikiwa kutetea kiti chake na kuibuka mshindi. Ni mbunge wa 46 wa CHADEMA. Msimamizi wa uchaguzi jimbo la mpanda Mjini Bw Henry Haule alimtangaza Alfi kuwa ni mshindi baada ya kupa kura 8,075 huku Sebastian Kapufi wa CCM akipata 8,020 na nafasi ya tatu ikienda kwa Aram Ndimubenya wa CUF aliyeambulia kura 39.

Katika Jimbo la Mpanda Vijijini, Moshi Kakoso wa CCM aliibuka mshindi kwa kura 5,693 akifuatiwa na Masanja Mussa wa CHADEMA aliyepata kura 3,260 huku nafasi ya tatu ikieda kwa Shaban Kisabo wa CUF aliyepata kura 74 na Makofila wa NCCR MAGEUZI kuibuka na kura 22.

Jimbo la Nkenge limechukuliwa na CCM. Pia Zanzibar, kati ya viti vinne, CUF imechukua vitatu, vikiwamo viwili ya Unguja. CCM imeambulia kimoja.

No comments:

Post a Comment