Wanachadema wamfagilia Nape Nnauye alipofika kumwakilisha Makamba kwenye mkutano mkuu wa Chadema
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akifurahi na mgombea urais, Dkt. willibrod Slaa baada ya kupitishwa kwa asilimia 99. 2 kuwani urais kupitia chama hicho
wanachama wakifurahia jambo kwenye ukumbi
Arcardo Ntagazwa akaribishwa rasmi
MKUTANO Mkuu wa Chama cha Demokrasia Maendeleo umempitisha rasmi kwa asilimia 99.2, Dkt. Willibrod Slaa kuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Wakipiga kura za ndiyo au hapana kwa kunyoosha mkono, wajumbe 752 kati ya 758 waliopiga kura, walikubali Dkt. Slaa abebe bendera ya chama chao katika mbio za kwenda ikulu, sita walisema hapana, baada ya kuulizwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe.
“Niko tayari kwa moyo wangu wote, kwa akili yangu yote na kwa nafsi yangu kamili kuwatumikia Watanzania, kadri matakwa ya Mungu yatakavyokuwa,” alisema Dkt. Slaa baada ya kupitishwa.
No comments:
Post a Comment