Thursday, August 26, 2010

CUF: Mambo 10 tutakayosimamia


Kuzindua ilani leo, kesho kampeni

Na Tumaini Makene

CHAMA cha Wananchi (CUF) kinatarajia kuzindua ilani yake leo, huku kikibainisha mambo kumi yatakayopewa kipaumbele iwapo kitapata ridhaa ya Watanzania kuongoza nchi katika Uchaguzi Mkuu 31, Oktoba mwaka huu.

Wakati kampeni za chama hicho zitazinduliwa kesho, leo Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba atazindua ilani ya chama hicho na kuifafanua mbele ya watu wa kada mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Prof. Lipumba ambaye pia ni mgombea urais wa CUF, anatarajiwa kufafanua vipengele hivyo 10, mbele ya viongozi wa taasisi mbalimbali za dini, vyama vya siasa, wasomi wa masuala mbalimbali, wanahabari na wananchi wengine wa kawaida.

Akizungumza na Majira jana Mkurugenzi wa Siasa wa CUF, Bw. Mbaralah Maharagande aliyataja masuala hayo 10 yatakayofafanuliwa na Prof. Lipumba kuwa ni pamoja na Serikali ya Umoja wa Kitaifa, chakula cha kutosha nchini ili akina mama na watoto wapate lishe bora. >>>Endelea Hapa.

No comments:

Post a Comment