Tuesday, May 04, 2010

Mugabe yuko Dar es Salaam

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Mheshimiwa Robert Mugabe, Rais wa Zimbabwe, amewasili nchini jioni ya leo, Jumatatu, Mei 3, 2010, kwa ajili ya mazungumzo na Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais Mugabe amelakiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa George Mkuchika kwa niaba ya Rais Kikwete.

Mara baada ya kuwasili Ikulu, Dar es Salaam, Rais Mugabe alilakiwa na mwenyeji wake, na viongozi hao walifanya mazungumzo ya faragha.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

03 Mei, 2010

No comments:

Post a Comment