Wednesday, May 26, 2010

Masaibu Gari la KikweteHili ndilo gari alilopansda Rais Jakaya Kikwete kwenye ziara yake Dar es salaam, likachomoka tairi muda mfupi baada ya kuteremka na kubadilisha gari. Ilikuwa hivi: Rais aliteremka akapandishwa gari jingine, baada ya kuondoka kuendelea na msafara, wakati gari hilo linawekwa pembeni tairi likakwanyuka kama picha inavyoonesha, katika eneo la BP, Kurasini Dar es Salaam. Hii ilikuwa mara ya pili ndani ya siku moja. Awali Rais alibadilisha gari katika eneo la Kimara, kwa matatizo mengine yaliyoelezwa ya kiufundi. (Picha kwa Hisani ya Gazeti la Majira)
Hapa gari hilo lilikuwa halijaondolewa nembo ya Mheshimiwa.
Habari hii ilistua watu wengi na vyombo vya habari juzi viliripoti namna hii, Majira: Magari ya JK yapata msukosuko. Jana wengine waliendelea kuifuatilia. The Citizen: Vehicles mishap: How safe is our president?

No comments:

Post a Comment