Tuesday, May 04, 2010

JK aamsha hasira

Nadhani watanzania tumejifunza jambo kwa hotuba hii ya kifedhuri. Walimu na watumishi wengine wanaolipwa mshahara wa kununua mchicha watafakari iwapo mchango wao unathaminiwa. Ni walimu wanaotumiwa na chama tawala kuiba kura na kuwaweka madarakani viongozi mafedhuri kwa kupewa khanga na chumvi. Fedha za Richmond, Epa na mabilion yanayochotwa kila siku yanatosha kuwalipa watumishi hao wanaolitumikia taifa hili kama watumwa.

Inauma sana na watanzania tunapaswa kufanya jambo juu ya hotuba hii ili iwe fundisho kwa rais na wenzake wenye tabia hiyo ya kutishia watu na maslahi yao.

MWITA BHOKE STEPHEH
TAMICO BRANCH SECRETARY
Ext.2639 Source Wanabidii

No comments:

Post a Comment