Tuesday, May 19, 2009

Ni nembo za vyama vitatu kati ya vinne vya siasa vinavyochuana vikali huko Busanda, wilayani Geita mkoani Mwanza. Juu kabisa ni Civic United Front (CUF), inafuata ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na ile ya Chama Tawala, CCM. Sikufanikiwa kupata nembo wala bendera ya United Democratic Party (UDP), kama kuna yeyote mwenye nayo, naomba anitumie, kupitia rsmiruko@yahoo.co.uk. Vyama hivyo vinashiriki uchaguzi mdogo wa kujaza kitiwazi cha ubunge Mei 24, 2009, kampeni za kupasua miamba zinaendelea, unaweza kutabiri matokeo ya uchaguzi huo kwa kura yako hapo kulia.

No comments:

Post a Comment